Kabendera Ataka Kujadiliana na DPP ili Kumaliza Kesi yake...


Jebra Kambole, Wakili wa mwandishi wa habari za Kiuchunguzi, Erick Kabendera ameijulisha Mahakama kuwa mteja wake anataka kujadiliana na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) namna ya kumaliza kesi inayomkabili

Wakili Kambole ameeleza hayo leo Oktoba 11, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu huku upande wa Jamhuri ukisema kesi hiyo ilikuwa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi haujakamilika

Baada ya Wankyo kueleza hayo, Kambole ameijulisha Mahakama taarifa kuhusu Kabendera kujadiliana na DPP kuwa ni kwa mujibu wa kifungu namba 194A(2) cha sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2019

Katika majibu yake, Wakili wa Jamhuri Simon Wankyo amesema jambo hilo ni kweli na wapo katika mchakato, akisisitiza kuwa taratibu zikikamilika wataipa taarifa Mahakama

Kabendera anakabiliwa na kesi ya Uhujumu Uchumi yenye mashtaka matatu likiwemo la utakatishaji wa zaidi ya Tsh. Milioni 173
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad