Kabla ya Kufikiria Harusi, Weka Haya Akilini!


WENGI wakiwaza kuhusu kufunga ndoa, mawazo yao huenda moja kwa moja kwenye namna sherehe ya harusi itakavyokuwa! Anataka gari kali la maharusi, ukumbi wa gharama, vyakula vya bei mbaya, wasanii maarufu wa kutumbuiza n.k.


Ni kweli ni vema kuifanya siku hiyo maalum na ya pekee maishani kuwa yenye kumbukumbu isiyofutika! Watu wanapenda kufanya sherehe kubwa ambayo itawafurahisha watu.



Katika kufanikisha hilo, huwa kunakuwa na kamati ya maandalizi ambayo ndiyo huratibu shughuli nzima. Katika kikao cha kwanza cha kuwaita wanakamati kuwaeleza nia yako ya kutaka kuoa, ahadi huwa nyingi sana.



Huyu atasema atagharamia gari la maharusi, mwingine atasema atasimamia usafiri wa wazazi, yule atasema mapambo nk, mradi kila aliyefika kwenye shughuli hiyo ya mwanzo wa maandalizi ya harusi ametoa ahadi yake.



Hapo huwa mwanzo wa mikikimikiki ya kukusanya fedha za michango na kuweka sawa mipango ya harusi. Ni safari ambayo huwa si ya chini ya miezi mitatu. Usipokuwa makini, kabla ya ndoa, bwana harusi anaweza kukonda kutokana na changamoto za kukimbizana na maandalizi.



Mwisho wake ni nini? Sherehe ya saa nne tu ukumbini, mamilioni yanakuwa yameshakatika. Kuna ishu nyingine ambayo vijana wanaotarajia kuoa huwa hawajiandai nayo kabla.



Baadhi ya watu huwa hawakamilishi walivyoahidi, mwisho wake unajikuta shughuli imekaribia na mambo hayajakamilika. Kwa kuwa lazima mambo yaende kama yalivyopangwa, ndipo bwana harusi mtarajiwa hujikuta akiingia kwenye mzigo wa madeni!



Yaani anachukua mke, anaanza naye maisha, badala ya kuanza na kuangalia maendeleo ya familia, anaanza kulipa madeni. Wakati mwingine madeni aliyojitengenezea yanaweza kuzalisha ugomvi ndani ya ndoa hiyo changa.



CHUKUA HII

Ndoa ina thamani kubwa kuliko sherehe ya kifahari ya saa chache. Sherehe yako haitakuwa na maana ikiwa ndoa itakuwa na migogoro. Mwanaume mjanja, hufikiria zaidi kumfurahisha mkewe, kuishi maisha ya amani na kuangalia maendeleo kuliko sherehe ya kifahari kwa lengo la kuwafurahisha watu.



Kama kweli uko vizuri, una fedha za kutosha, unaweza kuandaa sherehe kubwa; au kama una marafiki wenye ushirikiano mzuri, ‘wasio na pesa za mawazo’ unaweza kufanya sherehe kubwa, muhimu usiruhusu sherehe iwe chanzo cha kukupotezea furaha baada ya kutumia fedha nyingi.



MIFANO HAI

Ipo mifano ya watu wengi maarufu duniani wenye fedha zao, ambao hufanya sherehe ndogo.

Unaweza kuita kikao kidogo cha watu wako wa karibu kabisa – marafiki na jamaa mnaoshirikiana kwa shida na raha, mkaandaa hafla ya kawaida tu ya watu wasiozidi 100 (kwa mfano) na ukaweka kumbukumbu nzuri kwenye maisha yako.

 NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO BONYEZA HAPA

Hii ni safu yetu sisi wanaume, kwa hiyo nimeongea kiume. Wanawake hata uwaeleze nini, hiki nilichokiandika hawawezi kukielewa. Nachukua time!

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad