Kampuni ya mawasiliano ya simu, Smart Telecoms imefunga biashara yake nchini Tanzania, baada ya kuwa katika soko kwa kipindi cha miaka 4.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kuwa Machi 2019 kampuni hiyo iliwasilisha ombi la kufunga biashara kwa haraka, ila ikaongezewa miezi 3 ili kuwapa muda wateja waliokuwa wamenunua vifurushi mbalimbali kuvimalizia.
Kampuni hiyo ilirithi wateja 528 kutoka kwa iliyokuwa Benson Informatics mwezi Juni 2015, lakini ilipofika Oktoba 2015 wateja hao waliongezeka na kufikia 1,800,169. Wateja hao walianza kupungua, na hadi Machi 2019 ilikuwa na wateja 132,400.