KENYA: Gari lililozama baharini likiwa na mama na mtoto limetolewa zikiwa zimepita siku 13 (Picha)



Gari lililozama baharini siku 13 zilizopita katika kivuko cha Likoni feri, mjini Mombasa pwani ya Kenya hatimae limetolewa. Hii ni baada ya kundi la maafisa wa kikosi cha jeshi la wanamaji wa Kenya na wapigambizi wa Afrika Kusini kufanikiwa kufikia gari hilo.



Miili ya Mariam Kighenda, 35, na Amanda Mutheu, 4, pia imeopolewa kutoka ndani ya maji.Jitihada hizo zimekuwa zikiendelea kujaribu kuopoa miili ya mama na mwanawe wa kike waliokuwemo ndani ya gari hilo wakati lilipozama kutoka kwenye kivuko hicho mnamo Septemba 29.



Sept 29: Gari dogo aina ya soloon lililoarifiwa kuwa na watu wawili ndani lazama katika kivuko cha Likoni

Sept 30: Mkurugenzi mkuu wa shirika la Ferry Bakari Gowa asema kwamba wataalam wamebaini kuwa gari hilo lilizama kima cha mita 60, hivyobasi kufanya kuwa vigumu kuliokoa.

Sept 30: Shughuli za uokoaji ambazo zimejumuisha maafisa kutoka vitengo vya Kenya Navy, Kenya Ferry, na wapiga mbizi wa kibinafsi zaanza.

Okt 1: Kivuko cha feri chafungwa kwa saa tatu ili kuruhusu utafutaji ulioendelea wa gari na miili ya waliokuwemo ndani.

Okt 2: Familia ya waathiriwa yalalamikia kujikokota kwa operesheni ya uopoaji miili ya waathiriwa.

Okt 2: Kikosi cha pamoja katika operesheni ya uopoaji kinasema kimegunuda sehemu lilipo gari. Hii ni baada ya kuyakagua maeneo kadhaa yalioshukiwa kuwepo gari hilo.

Okt 3: Maafisa wanaendelea kushughulika na ukaguzi wa maeneo yalioshukiwa kuwepo gari hilo.

Okt 7: Wapigambizi wa Afrika Kusini wajiunga katika operesheni hiyo ya uopoaji.

Okt 8: Wapigambizi waanza kazi ya kutafuta miili na gari.

Okt 9: Gari lililokuwa limezama katika kivuko cha Likoni limeonekana. Msemaji wa serikali Cyrus Oguna asema haiwezi kuthibitishwa iwapo ndilo gari lililozama Jumapili Septemba 29.

Chanzo BBC

By Ally Juma.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad