Kigogo Usalama Mtuhumiwa wa Madawa Akosa Dhamana


OFISA Usalama wa Shirika la Posta Tanzania, George Mwamgabe (44) na dereva Abraham Msimu (54) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na makosa mawili likiwemo la kusafirisha madawa ya kulevya aina ya bangi gramu 124.55.



Washitakiwa hao wamesomewa mashitaka yao na Wakili wa Serikali, Adolf Lema, mbele ya Hakimu Mkazi, Augustina Mbando.



Katika shitaka la kusafirisha bangi, wanadaiwa kulitenda Agosti 25, 2018,  katika eneo la Posta Dar es Salaam.


Kosa la pili ni la kusafirisa dawa za kulevya aina Heroine Hydrochloride zenye uzito wa gramu 1.55 ambapo wanadaiwa walilitenda pia Agosti 25, 2018 katika jiji la Dar es Salaam.



Kwa pamoja washitakiwa hao wamekana makosa hayo na upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika. Washitakiwa hao wameomba wapatiwe dhamana ambapo mahakama imewapa masharti ya kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Sh. mil tano kila mmoja na mmoja wa wadhamini awe mtumishi wa serikali.



Washtakiwa hao wameshindwa kutimiza masharti hayo, hivyo wamerudishwa rumande na kesi imeahirishwa hadi Oktoba 16, mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad