Kikwete Katoa Ufafanuzi Juu Ya Upotoshaji Unaofanywa na Baadhi ya Watu Kuhusu Hotuba Yake
0
October 11, 2019
Ofisi ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete imetoa taarifa ya masikitiko juu ya upotoshwaji uliofanywa na baadhi ya Watu kuhusu hotuba aliyoitoa kwenye Kongamano la Mwalimu Nyerere.
“Mada ya kongamano ilikua Urithi wa Mwl. Nyerere katika Uongozi, Maadili, Umoja na Amani katika ujenzi wa Taifa, katika hotuba yake Rais Mstaafu Kikwete alielezea jinsi alivyomfahamu Mwl. Nyerere, kilichotushangaza na kutusikitisha sisi na Rais mstaafu ni kujitokeza Watu wanaopotosha ukweli kuhusu maneno aliyosema Rais mstaafu JK
“Tunapenda kusisitiza kuwa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kamwe hakuzungumzia Mtu mwingine yeyote zaidi ya Mwl. Nyerere na hakufanya ulinganifu Kati ya Mwl. Nyerere na Marais waliofuata baada yake, waliostaafu na waliopo sasa, katika hotuba yake hakutaja jina la Mtu yoyote hivyo tunaposikia wakidai Rais mstaafu alikua anasema Mtu ni jambo lililotusikitisha na kutusononesha, ni uzandiki fitna na uchonganishi
“Rais mstaafu alitazamia sana sana Watu wamkosoe kwa yale aliyoyasema kuhusu Mwalimu Nyerere na siyo kusingiziwa mambo ambayo hakusema, amewataka Watu wenye maoni yao wawe jasiri kuyasema na waache tabia ya kujificha katika kivuli cha hotuba yake
Tags