KIMENUKA..Askofu Awashukua Wachungaji Wanaodangaya Waumini Kwa Kutumia Mafuta, Chumvi na Maji Kuwaponya



ASKOFU wa Kanisa la Morovian Jimbo la Magharibi, Ezekiel Yona, amewataka wachungaji na mashemasi wa kanisa hilo kutojihusisha na vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na baadhi ya wana maombi ambao wamekuwa wakitumia chumvi, maji na mafuta kuwahadaa waumini.

Kauli hiyo aliitoa juzi wakati wa hafla maalumu ya kuliweka wakifu wa jengo jipya la kanisa la Morovian Jimbo la Kahama Mjini pamoja na kuwasimika mashemasi na makasisi 17.

Alisema wako baadhi ya viongozi wa dini wamekuwa wakiwadanganya waumini kutumia chumvi, maji, mafuta na kubusu kinywa cha nguruwe wanapofanyiwa maombi kwamba anaponunua na kuvitumia, anaweza kupona matatizo yake jambo ambalo si kweli.

"Baadhi ya watoa huduma za maombi kwenye madhehebu mengine wanaowanywesha mafuta waumini wao na kisha wanaanguka chini kwa kugalagala na baadaye wanawaombea na kuamka. Vitendo hivi msivifanye na havikubaliki katika kanisa la Mungu," alisema.

Askofu Yona aliwataka makasisi kuendelea kuliombea taifa ili amani iendelee kudumu na kumwombea Rais John Magufuli ili aendelee kuwatetea wanyonge sambamba na kurudisha nidhamu serikalini kwa kusimamia rasilimali za nchi.

Mmoja wa makasisi wapya waliopewa daraja hilo, Emmanuel Sangosango kutoka Kanisa la Morovian kituo cha Mwanza, alisema atahakikisha anakuwa mwaminifu kwa waumini wake na kujiepusha na maombi ya kutumia mafuta na maji.

Naye Yona Mbogo kutoka Singida, alisema atahakikisha anawaelekeza watoa maombi ambao wana tabia ya kuwadanganya waumini juu ya vitu hivyo na kubusu kichwa cha nguruwe ili wapone maradhi, huku wengine wakigeuza maombi kama biashara.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Asante askofu. Inahuzunisha hizi Imani potofu zinapopewa nafasi. Wanaozitetea wanadai eti walipata majibu ya mahitaji yao kupitia njia hiyo potofu. Swali kwao je maandiko hayakusema mtaweka mikono juu ya wagonjwa nao watapata afya? Sasa hayo ya maji, nguruwe yametoka wapi? Hata kahaba akifanya uasherati wake hupata kipato na na mahitaji yake muhimu yanajibiwa kwa kupitia kipato hicho mfano mahitaji ya chakula, nguo Kodi ya nyumba na mengine. Lakini kimaandiko hatukuambiwa tufanyeje kazi ya ukahaba hata kama inalipa. Ndugu zangu mnaodanganya watu na mliokubali kwa hiyari yenu kudanganywa,, kutii neno la Mungu ni bora. Itakufaa nini kupata uliwengu wote na kuukosa uzima wa milele? Je haikuandikwa jicho lako likikukosesha ling'oe? Ni heri uingie mbinguni ukiwa na jicho moja. Je Leo ukiambiwa ukahaba ni tiba ya maradhi yakusumbuayo utaamua kuingia ukahaba ili mradi kasema mchungaji wako au anayejiita nabii wakati maandiko yamekukataza?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad