Kiongozi wa upinzani Democratic Alliance ajiuzulu


Kiongozi wa kwanza mweusi wa chama rasmi cha upinzani Afrika kusini amejiuzulu kufuatia mzozo unaotokana na ubaguzi wa rangi ndani ya chama chake Democratic Alliance.

Mmusi Maimane amesema chama hicho hakiweza tena kuwa chombo stahiki kwa malengo yake ya kuwepo taifa lenye umoja.

Maimane ameeleza kwamba alipata tabu katika kukifanya chama hicho ambacho kwa muda mrefu kimekuwa na wafuasi weupe wa kiberali - kuwavutia wapiga kura weusi.

"Nitajiuzulu kama kiongozi wa DA... lakini nitasalia kama mbunge," amesema.

Mmusi Maimane: Mpinzani halisi ama ‘kibaraka wa Wazungu’?
Afrika Kusini: Meya mweusi ajiuzulu
Julius Malema - Mweka ajenda kali Afrika kusini
"Kuna muda wa viongozi kukaa kando na kufanya ukaguzi wa kisawasawa," aliongeza.

Kujiuzulu kwake kunajiri siku tatu baada ya Herman Mashaba kujiuzulu kutoka chama hicho na pia kama meya wa mji wa Johannesburg.

Hii inafuata uteuzi wa kiongozi wa zamani wa chama hicho, Helen Zille, kama mwenyekiti wake, na wadhifa wa pili wenye nguvu ndani ya chama hicho.

Maimane alizozana na Bi Zille mnamo 2017 baada ya Zille kutukuza kwa kiasi fulani utawala wa kikoloni.

Kituo cha televisheni nchini kimeweka video ya tangazo la Maimane kujiuzulu:
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad