Kitambulisho cha Taifa, kupigia kura havitahusika uchaguzi wa serikali za mitaa
0
October 10, 2019
Serikali Mkoani Pwani, imetoa rai kwa wananchi kupuuza baadhi ya watu wanaowahadaa kuwa kitambulisho cha Taifa -NIDA na cha kupiga kura wataweza kupigia kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa,vitongoji na vijiji Novemba 24 mwaka huu,suala ambalo ni upotodhaji mkubwa.
Aidha imeweka bayana takriban watu 680,000 wanatarajiwa kujiandikisha kwenye daftari hilo, hivyo wamehamasishwa kujiandikisha ili kuwa na haki ya kupiga kura kuchagua viongozi wanaowataka.
Akihamasisha umuhimu wa kujiandikisha katika daftari hilo hadi octoba 14 mwaka huu ,wakati alipokwenda kutimiza haki yake ya msingi kujiandikisha kituo cha Mwanalugali ‘A ‘ Kibaha ,mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo alisema kitambulisho cha Taifa na cha kupigia kura havitahusika katika zoezi la kupiga kura.
“Nimetumia haki yangu ya msingi kujiandikisha ,nimejiandikisha wa 123 lengo la kituo hiki ni kuandikisha watu 1,332 na kimkoa tunatarajia kuwa na watu 680,000 ,alifafanua Ndikilo.
“Wapo baadhi ya watu wanahadaa wenzao kwamba hakuna ulazima wa kujiandikisha kwenye daftari la wakazi na badala yake watatumia vitambulisho kama si cha uraia basi cha kupiga kura,sio kweli mtapoteza haki yenu ya msingi.”
Hata hivyo Ndikilo alieleza ,suala la kupiga kura ni la wananchi wote siyo la watu wachache ili kuondoa malalamiko kuwa viongozi waliochaguliwa hawafai wakati wao hawakushiriki hilo ni tatizo.
Alisema taratibu zote zimekamilika ikiwa ni pamoja na fedha ambapo wasimamizi tayari wameshateuliwa kwa ajili ya uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Novemba 24 mwaka.
Tags