Kiwango cha maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kitaifa kimeshuka kutoka asilimia 7 mwaka 2003/04 hadi kufikia asilimia 4.7 2016/17 huku maambukizi kwa wanaume ikiwa ni asilimia 3.4 na wanawake ni asilimia 6.3
Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Zainab Chaula akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya mpango wa taifa wa kudhibiti Upungufu wa Kinga Mwilini (UKIMWI) ya mwaka 2018/19 mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge
Kiwango hicho cha maambukizi kimeonekana kushuka kufuatia utafiti wa hali ya maambukizi nchini na kudai kuwa Wizara kupitia NACP inatekeleza mpango mkakati wa kupambana na UKIMWI na unapaswa kufikiwa ifikapo mwaka 2020
Katika kipindi cha kuanzia 2015 hadi Juni, 2019 Serikali imetekeleza hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na huduma za ushauri nasaha na upimaji, huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU
Huduma zingine ni za tohara ya kitabibu kwa wanaume, huduma za kondomu, huduma za VVU na UKIMWI kwa makundi maalumu na huduma za Habari, Elimu na mawasiliano ya kubadili tabia