Kocha Simba Ataja Ushirikina wa Mabao ya Kagere


KOCHA Mkuu wa Simba, Kocha Simba ataja ushirikina wa mabao ya Kagereamefunguka kuwa hana imani kuwa ushirikina unahusika kwenye mabao ya mshambuliaji wake, Mnyarwanda, Meddie Kagere.



Kauli hiyo aliitoa mara baada ya mshambuliaji huyo kuwa na mwendelezo mzuri wa kufunga mabao tangu kuanza msimu huu wa Ligi Kuu Bara ambao amecheza michezo mitano huku akifumania nyavu mara saba.


Mshambuliaji huyo juzi alifikisha bao la saba wakati walipocheza na Azam FC kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam huku wakifanikiwa kushinda bao 1-0 lililofungwa na yeye mwenyewe ambapo kasi yake imekuwa ikisababisha baadhi ya mashabiki kuhusisha na nguvu ya ziada kwa mchezaji huyo.



Akizungumza na Championi Ijumaa, Aussems alisema kuwa hakuna siri yoyote ya mabao ya Kagere wala ushirikina huku akifurahishwa na kasi yake ya kufunga mabao kwenye michezo mitano mfululizo waliyocheza.



Aussems alisema ni ngumu Kagere kumdhibiti asiifunge timu pinzani kutokana na mbinu nyingi alizonazo kwa mabeki wa timu pinzani.



“Kagere ni muuaji wa kimyakimya ambaye yeye ukimuacha, basi hakuachi ni lazima akudhuru kutokana na aina yake ya uchezaji kwenye goli la wapinzani.



“Na ili asifunge, basi muda wote umkabe kwa lengo la kutomuachia nafasi ya kufunga, hivyo ni lazima mabeki wakae naye karibu kitu ambacho ni kigumu, ni lazima watamsahau na ndiyo hapo utamuona Kagere anafunga bao.



“Hivyo, hakuna siri yoyote aliyonayo Kagere ya nje ya uwanja, kwanza mimi sitaki kuamini ushirikina kama ulivyoona mechi na Azam FC mabeki wa timu hiyo muda wote walikuwa karibu, lakini walimsahau kidogo akawafunga.



“Kagere ni aina ya washambuliaji ninaowahitaji katika timu yangu, nimepanga kusajili mshambuliaji mwingine mwenye uwezo zaidi ya wake katika dirisha dogo,” alisema Aussems.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad