Kondoo 2,000 Wasababisha Foleni Katikati ya Jiji


KATIKA hali isiyo ya kawaida, zaidi ya kondoo elfu mbili (2,000) wamekatisha katikati ya jiji la Madrid nchini HIspaia, jana Jumapili, Oktoba 20, 2019.


Hii ni sehemu ya makubaliano ya mwaka 1994, kwa wafugaji kuwa na haki ya kukatisha katikati ya jiji hilo kipindi kama hiki wakiwa na wanyama wao na kukatiza njia hizo ambazo zilikuwa za jadi hapo nyuma.


Safari ya wanyama hao ilianzia eneo la Casa de Campo ilipokuwa ni sehemu ya mawindo,  na kukatiza makao makuu ya benki ya Hispania wakielekea nje ya mji.


Safari hiyo ilisababisha foleni na msongamano lakini baadhi ya raia walipata muda wa kupiga picha na kuwapa chochote wanyama hao.


Tukio hilo ambalo lilianza mwaka 1994 linawapa haki kondoo na mifugo mingine kutumia njia hizo ambazo walikuwa wakizutumia miaka hiyo kabla ya mji kupanuka ambapo walikuwa wakikatiza msimu wa baridi kwenda kupatiwa malisho wakitokea kaskazini mwa Hispania.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad