Korea Kaskazini yafyatua kombora zito, linaweza kubeba nyuklia
0
October 03, 2019
Korea Kaskazini imethibitisha kuwa jana, Oktoba 2, 2019 imefanya jaribio la kombora zito lenye uwezo wa kubeba nyuklia, linalodaiwa kufanikiwa zaidi tangu Mei, 2019.
Kombora hilo ambalo taarifa zake zilitangazwa na kituo cha habari cha Korea Kaskazini, ni jaribio la 11 kwa mwaka huu.
Aidha, Jaribio la kombora hili limekuwa la kipekee kwani limefanywa kutoka kwenye boti maalum ya kijeshi yenye uwezo wa kuzama ndani ya bahari na kushambulia. Hivyo, limekuwa na uwezo wa kushambulia kirahisi hata nje ya mipaka ya nchi hiyo.
Kwa mujibu wa Maafisa wa Korea Kusini, kombora hilo limeruka umbali wa Kilometa 450 ardhini na kufikia umbali wa altitude 910 juu kabla haijaanza kushuka na kuangukia baharini.
Kombora hilo liliangukia kwenye eneo la bahari la Japan ambalo pia huitwa Bahari ya Mashariki. Japan imethibitisa kuwa kombora hilo lilitua kwenye eneo lake ambalo inaliita eneo maalum la kiuchumi.
Jaribio hilo lilifanyika saa chache tangu Korea Kaskazini ieleze kuwa ina mpango wa kurejea mezani kufanya mazungumzo na Marekani kuhusu nyuklia.
Kombora hilo lilifyatulia kutoka baharini Jumatano, Oktoba 2, 2019 kwa saa za nchi hiyo.
Tofauti na majaribio mengine mengi, kiongozi wa taifa hilo, Kim Jong Un hakuwa kwenye picha inayoonesha jaribio hilo.
Maafisa wa Korea Kaskazini wamesema kombora hilo ni kwa ajili ya kujilinda pamoja na kusababisha hatari kwa adui wa nje.
Tags