Korea Kaskazini Yathibitisha Kurusha Kombora Hatari Zaidi


Korea kaskazini imethibitisha kufanya jaribio la kurusha aina mpya ya kombora, baada ya kufanikiwa kurusha makombora ya masafa mafupi tangu mwezi Mei.

Jaribio hili nchini humo ni la kumi na moja kwa mwaka huu ambapo makombora yenye uwezo wa kubeba silaha za nyuklia yanarushwa.

Lakini utofauti wa jaribio hili ni kuwa, kombora halijarushwa kutoka ardhini, bali kwenye nyambizi chini ya bahari.

Kombora hili kuwa na uwezo wa kurushwa kutoka majini ni umuhimu zaidi kwa nchi hiyo kwa kuwa sasa wanauwezo wa kufanya mashambulizi mbali ya eneo lao.

Kwa mujibu wa maofisa wa Korea Kusini, kombora hili lina uwezo wa kuruka kwa kasi ya km 450 na kufika urefu wa km.910 kabla alijashuka baharini.

Hii ina maanisha kuwa makombora haya yana uwezo wa kuruka umbali mrefu mara mbili wa kiwango cha kimataifa ingawa makombora ya awali ya Korea Kaskazini yalikuwa na uwezo wa kuruka mbali zaidi.

Kombora hilo liangukia baharini upande wa Japani, unaoitwa upande wa mashariki wa bahari.

Japani imedai kuwa kombora hilo limetua katika umbali wa kilimita 200 kutoka ardhi yake. .

Jaribio hilo linakuja muda mfupi baada ya Korea Kusini kusema kuwa mazungumzo ya nyuklia kati yao na Marekani yataendelea.


Makombora hayo yalizinduliwa baharini siku ya Jumatano majira ya saa saba usiku saa za Afrika mashiriki, kilomita 17 kaskazini mashariki mwa fukwe za mji wa Wonsan .

Ripoti kutoka televisheni ya taifa hilo KCNA imesema kuwa leo Alhamisi, majaribio matatu kutoka juu yatarushwa ," makombora haya yamebuniwa kutoa vitisho kwa mataifa mengine na kujilinda".

KNCA imeongeza kuwa hakuna madhara yatayotokea kwa nchi za jirani.

Tofauti na majaribio ya awali hakukuwa na picha ya rais Kim Jong-un katika uzinduzi .

Katika majaribio kumi ya awali ya kurusha makombora mwaka huu, ni makombora la masafa mafupi tu ndio yaliorushwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad