Bondia aomba radhi kwa kusema atamuua mpinzani wake



Bondia wa Uingereza, Dereck Chisora ameomba radhi kwa kusema atamuua mpinzani wake David Price.

Kauli hiyo ameitoa siku tisa tu baada ya bondia wa Marekani Patrick Day kufariki akiwa na umri wa miaka 27 baada ya kusumbuliwa na majeraha ya ubongo aliyoyapata wakati anapambana.

 Akiongea kwenye mkutano na wanahabari kabla ya pambano la uzani wa juu litakalofanyika Jumamosi katika ulingo wa O2 Arena, Chisora, mwenye miaka 35, alisema neno la kuua lilimponyoka.

Day alipoteza fahamu baada ya kupigwa kwenye raundi ya 10 na Charles Conwell kwenye pambano la super welterweight Oktoba 12 huko Chicago, na kufariki baada ya siku nne.




Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad