Kuzimia Kwa WEMA Mara Kwa Mara Kukondeana Kwake Kwahusishwa

Fahamu: Usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita Wema alianguka na kupoteza fahamu usiku wa manane akiwa kwenye sherehe yake ya kuzaliwa (private party) iliyofanyika nyumbani kwa dada yake, Nuru Sepetu maeneo ya Mbezi-Beach jijini Dar. .
.
Achana na tatizo la kukondeana linalozungumzwa na wengi, gazeti la Risasi limeeleza kwamba hii ni mara ya tatu kwa sweetheart huyo kuzimia katika siku za hivi karibuni. Kufuatia tukio hilo la Jumapili kulizuka taharuki kubwa kwa wageni mbalimbali waliofika nyumbani hapo. .
.
Chanzo makini kililiambia Risasi kuwa, sherehe hiyo Wema alifanyiwa kwa kushtukizwa bila yeye kufahamu ambapo walioshiriki ni rafiki na ndugu wa karibu, jambo ambalo lilimfurahisha mno Wema na badaa ya kufurahi huku vinywaji vikiendelea ndipo lilipotokea tukio hilo la kusikitisha kwa kuzimia .
.
“Unajua Wema alikuwa na furaha iliyopitiliza na wakati wote hakupenda kukaa wala kufanya chochote, badala yake alikuwa akipita huku na huku kuzungumza na rafiki zake ndipo alipojisikia vibaya na kudondoka kisha kuzimia ambapo ilibidi akimbizwe hospitalini kwa huduma ya kwanza ambapo aligundulika alikuwa na presha ya kushuka,” mpashaji huyo aliliambia Risasi .
.
Pamoja na kadhia hiyo, lakini bado watu waliendelea kuisherekea siku ya kuzaliwa ya staa huyo mkubwa huku wakimiminia zawadi na muziki ukiendelea mpaka staa huyo alipopatiwa matibabu na kurejea nyumbani salama

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad