Lissu Atilia Mkazo Nia Yake ya Kugombea urais 2020


Mwanasiasa na mwanasheria wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, ametilia mkazo nia yake ya kugombea urais 2020, endapo atapata wito kutoka kwa wananchi na chama chake kugombea nafasi hiyo.

Lissu ametoa msisitizo huo alipozungumza na chombo cha habari cha VoA, alipokuwa nchini Marekani na kueleza kipaombele chake endapo atapata nafasi hiyo.


” Nimeshatangaza utayari wangu wa kugombea nafasi hiyo nikiteuliwa na chama changu na ninarudia tena nikipata wito wa kugombea urais nitapokea wito huo.” amesema Lissu

Lissu ambaye yupo nje ya nchi tangu mwezi Septemba 7, mwaka juzi kwaajili ya matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi ameshikilia msimamo wake huo wa kugombea urais licha ya hivi karibuni kubainisha kuwa hatarejea nchini hadi hapo chama chake kitakapo mhakikishia usalama wake.

Wanafunzi watano wafa maji Morogoro
Ametaja malengo yake iwapo atafanikiwa kuteuliwa na chama chake kugombea urais, amesema atarejea upya mchakato wa kutengeneza katiba mpya ya wananchi ili kuwapatia wananchi katiba bora.

Lissu amekuwa Mbunge kwa vipindi viwili, alivuliwa ubunge wake mwaka huu kutokana na sabau ambazo spika wa bunge, Job Ndugai alizitoa za utoro bungeni na pia kutokujaza fomu za maadili ya watumishi wa umma ambazo hutakiwa kujazwa pia na wabunge wote.
Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tundu Anthpas Lissu, mimi nataka ujue
    kuwa nchi yetu imetoka katika ya kupambana na kuziba mianya ya mazingira ya Hewa Hewa.

    Unafikiri Nchi itakuwa Tayari kumwingiza katika kinyanganyiro mtu ambae mgonjwa akijulikana FULL HEWA KAMA YOTEEEE.Jitathmini kwenye nywele.

    Ukujua hakuna Ubunge Hewa
    Ukijua Hakuna URAISI HEWA...!!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mie nilijua atapokelewa kitengo cha Moi.
      Lakini ni Dhahiri kwamba apokelewe na Dr.Nkya huko jijini
      Dodoma. manake hii ni mihemuko ya kudumiwa na kupata Tiba ya MIREMBE.
      MUUGHWAI ANTIPHAS LISSUKUOTA ULAHISI NIKIOJACHA MCHANA ULIO TANDA WINGU LA MASIKA.

      HIVYOUKO CHAMA GANI MANAKE HUJALIPIA ADA YA UANACHAMA NA KADIYAKO IMESITISHWA, JE UAYO TAARIFA HAMNAZO WEWE.!!

      Delete
    2. Mie nilijua atapokelewa kitengo cha Moi.
      Lakini ni Dhahiri kwamba apokelewe na Dr.Nkya huko jijini Dodoma.

      Manake hii, ni mihemuko ya kuhudumiwa na kupata Tiba ya MIREMBE.

      MUGHWAI ANTIPHAS LISSU, KUOTA ULAHISI NI KIOJA CHA MCHANA, ULIO TANDA WINGU LA MASIKA.

      HIVYO UKO CHAMA GANI? MANAKE HUJALIPIA ADA YA UANACHAMA NA KADI YAKO IMESITISHWA. JE UAYO TAARIFA? HAMNAZO WEWE.!!

      Saizi yako ni uje tulime sanflawa Inalipa iki Itawapendeza milembe.
      Au ajira ya kiwanda toka Mia 9 itapendeza. Kalibu

      Delete
  2. Tundu Anthpas Lissu, mimi nataka ujue
    kuwa nchi yetu imetoka katika ya kupambana na kuziba mianya ya mazingira ya Hewa Hewa.

    Unafikiri Nchi itakuwa Tayari kumwingiza katika kinyanganyiro mtu ambae mgonjwa akijulikana FULL HEWA KAMA YOTEEEE.Jitathmini kwenye nywele.

    Ukijua hakuna Ubunge Hewa
    Ukijua Hakuna URAISI HEWA...!!!

    ReplyDelete
  3. Insikitisha...!!!
    Mpaka Hosphuko Ughaibuni ..Umeendeleza
    Sera ya Utoro na kuingia mitini.

    Mbogo bana. BADILIKA MAGUMASHI.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad