Magufuli Ajutia Kuwa Rais "Hii ni Kazi Ngumu SANA Hata Mawaziri Hawajui Kesho Yao"



RAIS John Magufuli amesema anajutia kwa kihelehela chake cha kujazafomu ya kugombea nafasi hiyo na amewaomba viongozi wa dini kumwombea kutoka na ugumu wa kazi alionayo

Magufuli amesema hayo leo Oktoba 4, 2019 wakati akiongea na wananchi wa mji Wa Mlowo mkoani Songwe kwenye ziara yake ya kikazi mkoani humo.

"Ndugu zangu kazi hii ni ngumu sana hata mawaziri wangu hawalali usingizi na hawajui kama kesho yake wataamka wakiwa katika nafasi zao," amesema.

Amesema kila unapoangalia kusonga mbele ujue kuna maadui sasa lazima tuchape kazi kwa kumtanguliza Mungu na wale waliojitoa ufahamu Mungu awasaidie.

"Eti mtu wa chama fulani anafurahia. ndege ya Tanzania kushikiliwa katika nchi nyingine, ninawaomba viongozi wa dini kubeba jukumu la kuliombea hilo," amesema Magufuli.

Pamoja na mambo mengine amesema serikali imetoa billion 18 kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe (SIA) na mkandarasi anaendelea na kazi, lengo likiwa ni kwa ndege kubwa kutua.

Vilevile rais Magufuli ameimiza upendo ,amani, ushirikiano kwa watanzania wote na kumtangyuliza Mungu kwa kila jambo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad