Mahakama ya rufaa imetengua uamuzi wa mahakama kuu uliozuia wakurugenzi kusimamia uchaguzi Tanzania
0
October 17, 2019
Mahakama ya rufaa ya Tanzania imetengua uamuzi wa mahakama kuu uliowazuia wakurugenzi wa manispaa, wa miji na wilaya kusimamia uchaguzi mkuu.
Uamuzi huo unakuja mwaka moja kabla ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo ambapo ilielezwa kuhusika kwa maafisa, walioteuliwa na rais - ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha siasa, kuwa ni hatua inayohatarisha uchaguzi kutokuwa wa huru na haki.
Uamuzi huo ulitokana na uamuzi wa mahakama kuu uliotolewa na jopo la majaji watatu, Dk Atuganile Ngwala, Dk Benhajj Masoud na Firmin Matogolo uliobatilisha kifungu cha 7(1) cha Sheria ya uchaguzi kinachoipa mamlaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwateua wakurugenzi wa miji, manispaa na wilaya kuwa wasimamizi wa uchaguzi.
Pia mahakama ya rufaa imebatilisha kifungu cha 7(3) kinachoipa NEC mamlaka ya kuteua mtu yeyote miongoni mwa watumishi wa umma kuwa wasimamizi wa uchaguzi.
Katika hukumu hiyo mahakama imeeleza kwamba vifungu hivyo ni kinyume cha katiba ya nchi, ikibainisha kuwa wakurugenzi hao huteuliwa na rais aliyeko madarakani ambaye hutokana na chama tawala na kwamba wengine ni wanachama wa chama cha mamlaka inayowateua, jambo ambalo huathiri utendaji wao katika kutenda haki.
Pia ilisema kwamba sheria haijaweka ulinzi kwa tume ya NEC kumteua mtumishi yeyote wa umma kuhakikisha kuwa anakuwa huru katika kutekeleza majukumu yake.
Tags