Makonda Awachana Mdee, Mnyika & Kubenea Amwomba JPM Bil 1.5


Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda amemuomba Rais Dk. John Magufuli ampatie Tsh bilioni 1.5, kwa ajili ya ujenzi hospitali ya Wilaya ya Ubungo ili kuwaondolea adha wakazi wa eneo hilo wanaolazimika kufata huduma za afya katika Hospitali za Wilaya nyingine zilizopo jijini humo.



Makonda amesema hayo leo Jumamosi, Oktoba 26, 2019, wakati akitoa salam za wakazi wa mkoa wake kwa Rais Dkt. John Magufuli katika mapokezi ya ndege mpya ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) aina ya Boeing 787-8 Dreamliner.



“Bahati mbaya sana kuna majimbo matatu ya Kibamba, Ubungo na Kawe… Dar es Salaam tulikosea kuchagua, wabunge hawa ni ‘wezi’, wanakula posho bungeni bila kufanya kazi za wananchi. Ubungo ina wabunge wawili na Meya wa upinzani hawawezi kuja kwenye shughuli za maendeleo wala kueleza changamoto za wananchi wao.



“Wameshindwa hata kuleta mpango kupitia RCC ili ijengwe hospitali ya wilaya ubungo, hata kutoa mawazo yao tu na kupaza sauri kwa ajili ananchi wao wameshindwa. Kwenye shughuli za maendeleo kama hizi huwaoni.



“Mhe Rais nikuombe jambo moja tu, Ubungo ni wilaya mpya lakini haina hata hospitali ya Wilaya, wananchi wa Ubungo wanalazimika kutumia hospitali ya Wilaya ya Kinondoni, ninakuomba unipatie shilingi bilioni 1.5 niwajengee hospitali ya wilaya ili waondokjane na hii adha,” amesema Makonda.



Ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 262 na uwezo wa kusafiri kwa takribani saa 18, tayari imeshatua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam ikitokea nchini Marekani ambako ilikuwa inaundwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad