Mamlaka ya Hali ya Hewa yatoa tahadhari
0
October 30, 2019
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini TMA imetoa tahadhari ya kuwepo kwa mvua kubwa katika Mikoa ya Mwanza, Geita, Kagera na sehemu ya Mkoa wa Simiyu.
Ikitoa utabiri huo wa siku tano kuanzia leo TMA imesema mvua hizo zitakazokuwa za wastani zinaweza kusababisha uharibifu wa barabara, madaraja na miundombinu mingine hivyo mamlaka zinazohusika zinatakiwa kuchukua tahadhari.
Hivi karibuni TMA iliripoti juu ya kutokea kwa mvua Ukanda wa Pwani Mikoa ya Tanga, Visiwa vya Unguja na Pemba ambayo ilileta madhara ikiwemo vifo na uharibifu wa mali.
Tags