Mapenzi ya Siku Hizi ya Kuviziana..Unajaribiwa Kwa Kuombwa Kitu
0
October 14, 2019
Unakutana na mdada....unajenga mazoea anakupa mawasiliano. Unajaribu kuwasiliana naye unaona kama hakupi muda kivile. Unajisemea aah labda hanipendi.
Kama mnavyojua moyo unamilango mingi...mmoja unakuambia labda umpe muda anakuzoea atakuwa poa baadae. Kabla hajakuzoea unaombwa kitu.
Kwa wenye akili kidogo unajishauri ndani ya dakika unamwambia sawa umekipata chukua. Ukishampa anaanza kukuchangamkia hadi unashindwa kuelewa imekuaje.
Sasa mimi maswali yangu kwa wadada ni haya.
Kabla sijawauliza naamini wa humu wapo wanaofanya wengine hawalifanyi hili. Na silalamiki nataka mtupe uzoefu.
1. Je, huwa mnapenda?
2. Kama jibu ni ndiyo huwa mnapenda. Kwanini switch ya upendo wenu inawashwa mkipewa mlichoomba?
3. Ok, tuseme mwanaume aliyeomba mawasiliano haujampenda na umetumia mbinu ya kumwomba kitu ili akukimbie. Sasa kwanini ukipewa unajipendekeza kwake saana hadi mwanaume anaanza kujistukia? Kama hukumpenda naamini huwezi badili moyo kwa kakitu kadogo.
4. Je, hii ni tabia ambayo ipo ndani ya mwanamke au ni ya kujifunza?
5. Je, mpo ambao mlikuwa hamifanyi na sasa mnaifanya? Kipi kilikufanya ukaanza kuifanya?
6. Je, mnapofanya hili mnakuwa na maana gani?
7. Mpo ambao hamfanyi hiki kitu? Nyie huwa mnafanyaje?
Nisiwe muongo nikikutana na hii hali kwanza huwa hivi...kwanza nakutumia meseji....akili inaniambia huyu labda hajanipenda nini? Najisemea acha nione ndani ya masaa mawili. Before unaombwa kitu...unatoa. baada ya kutoa unachangamkiwa...
Najiuliza mambo mengii hadi naanza kuwaza ujinga mwingine maana jibu nabaki sina.
Tags