Marekani yapiga marufuku kampuni za China kwa unyanyasaji wa Waislamu
0
October 08, 2019
Marekani imepiga marufuku mashirika 28 ya China kwa madai ya kuhusika katika unayanyasi wa kabila la Uighurs katika jimbo la Xinjianga nchini China.
Mashirika hayo sasa yameorodheshwa miongoni mwa yale yaliopigwa marufulku na taifa hillo hatua inayoyazuia kununua bidhaa kutoka kwa makampuni ya Marekani bila idhini ya Washington.
Mashirika hayo yaliolengwa yanashirikisha mashirika ya serikali na kampuni za kiteknolojia zinazoshughulika na vifaa vya ujasusi.
Mnamo mwezi Mei , utawala wa rais Trump uliiweka kampuni kubwa ya teknolojia Huawei katika orodha jhiyo kutokana na hofu ya kiusalama kuhusu bidhaa zake.
Idara ya biashara imesema kwamba mashirika hayo yanahusika na ukiukaji wa haki za kibinadamu na unyanyasaji.
Mashirika ya haki za kibinadamu Beijing yanasema kwamba mashirika kadhaa yananyanyasa Waislamu wa kabila la Uighurs katika kambi za vizuizi .
China imevitaja vituo hivyo kuwa vya kukabiliana na watu wenye itikadi kali.
Idara hiyo ya biashara imesema katika uamuzi wake siku ya Jumatatu kwamba mashirika hayo 28 yanahusika katika kampeni ya China ya ukandamizaji , kuwakamata na kuwazuia watu kadhaa na ujasusi wa hali ya juu dhidi ya Uighurs, Kazaks pamoja na makundi mengine ya Waislamu walio wachache.
Shirika la usalama wa umma la Xinjiang pia lipo katika orodha hiyo pamoja na mashirika mengine 19 madogo madogo.
Kampuni za Hikvision, Dahua Technology na Megvii ni miongoni mwa mashirika manane ya kibiashara yaliopo katika orodha hiyo , yote ambayo yanaangazia utambuzi wa sura ya mtu.
Hikvision ni mojawapo ya kampuni ilio na vifaa vikubwa vya uchunguzi duniani.
Marekani na China zipo katikati ya mgogoro wa kibiashara na zimetuma ujumbe Washington kwa mkutano kuhusu wasiwasi uliopo kati yao wiki iliopita.
Marufuku hiyo pia inalenga kampuni ya China ya AI stars
Hatua hiyo ya Marekani bila shaka itaathiri maono ya kiteknolojia ya China hata iwapo kwa muda mfupi.
Kampuni ambazo zinalengwa ni baadhi ya kampuni kubwa za teknolojia nchini China - sekta ambayo China inalenga katika siku za usoni.
Hatahivyo Algorithm inayotumika katika mafunzo ya AI kwa sasa hutengezwa na kampuni za Marekani pekee kama vile Intel, Movidius na Nvidia.
Hatahivyo hatua hiyo inaishinikiza Marekani kuanza kujitegemea katika utengenezaji wa bidhaa hizo.
Kwa mfano baada ya Huwawei kuorodheshwa katika orodha hiyo ya Marekani mapema mwaka huu hatua iliomaanisha kwamba kampuni kama vile Google zitahitaji kupata leseni ya kuuza nje kutoka kwa Washinton kabla ya kuuza - kampuni hiyo ya China ilisema kwamba itaanza kutengeza programu zake kuweka katika simu zake.
China pia inaendelea kutengeza programu za Marekani ili kujikimu katika kampuni zake za teknolojia.
Huku vita vya kibiashara kati ya marekani na China vikiongezeka kuhusu teknolojia, wateja watahitajika kuchagua kuhusu bidhaa zilizotengezwa China na zile zilizotengezwa Marekani.
Tags