Mbelgiji wa Simba Kumpeleka Kagere Burundi

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba wamepanga kwenda nchini Burundi kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Aigle Noir.

Simba inayofundishwa na Mbelgiji, Patrick Aussems, hivi sasa inaongoza kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 12 ikicheza michezo yake yote minne.

Ligi inatarajiwa kupumzika kwa siku chache kupisha maandalizi ya timu ya taifa, Taifa Stars inayojiandaa na mchezo wake wa kufuzu Chan dhidi ya Sudan.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatatu na kuthibitishwa na Meneja Mkuu wa timu hiyo, Patrick Rweyemamu, kocha ndiye aliyependekeza kucheza michezo miwili ya kirafiki kabla ya kurejea Bongo kucheza na Azam.

Rweyemamu alisema kuwa lengo la kucheza michezo hiyo ya kirafiki ni kuwaongezea mechi fitinesi wachezaji wake akiwemo Meddie Kagere ili watakaporejea kwenye ligi wawe fiti.

Aliongeza kuwa mchezo wake wa kwanza atakaocheza ni dhidi ya Mashujaa FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza hapa nchini kabla ya kwenda kucheza na Aigle Noir watakapokwenda Burundi.

“Kama unavyofahamu timu ikifanya mazoezi bila ya kucheza mechi, kocha anashindwa kuona upungufu wa kikosi chake pamoja wa wachezaji kukosa mechi fitinesi.

“Hivyo, kocha alipendekeza wakati ligi ikisimama kwa wiki mbili kupisha maandalizi ya timu ya taifa, amependekeza tucheze mechi hizo mbili za kirafiki kabla ya kurejea kwenye ligi kucheza na Azam.

“Michezo tutacheza miwili, kati ya hiyo mmoja wa kimataifa tutakaocheza huko Burundi dhidi ya Aigle Noir na baadaye Mashujaa ya hapa nchini inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza,” alisema Rweyemamu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad