'Mbeya si ya watu ambao ni wambea' - Chalamila

 
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila, amesema wakati anachaguliwa kuwa Mkuu wa Mkoa, lengo lake la kwanza lilikuwa ni kuhakikisha Mkoa huo unakuwa na watu wanaowajibika kwa kufanya kazi,jambo ambalo anaona linaenda vizuri.


Chalamila ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na EATV na EA Radio Digital,na kueleza kwamba atahakikisha anacharaza viboko, vikundi vya watu ambavyo atavikuta vimekaa kijiweni vikiisema Serikali.

"Hizi bakora zitaendelea nikikuta kikundi cha watu wanaisema Serikali, basi nitatumia watu wa namna hiyo nitawaonya kwa njia hiyo, tunataka Mbeya hii iwe Mji salama kwa watu wake"  amesema Chalamila.

"Nataka Mbeya hii iwe salama, Mbeya hii inaitwa Mbeya si kwa sababu una wambeya bali nataka imaanishe kuna watu wanaojielewa na ni kweli wengi wao wapo hivyo na naamini tutafikia tunachokitaka" amesema RC Chalamila.

Hivi karibuni Mkuu huyo wa Mkoa akizungumza na EATV na EA Radio Digital, alieleza kwa utafiti mdogo alioufanya amegundua asilimia kubwa ya watu, wanaoikosoa Serikali wengi wao hawako kwenye mahusiano.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad