Mbunge wa Moshi Mjini agoma kugombea tena 'nimeshaamua mwaka 2020 nitapumzika'

Mbunge wa Moshi Mjini (CHADEMA)  Japhary Michael tangu mwaka 2015 alipomrithi Philemon Ndesamburo aliyeshika jimbo hilo kwa vipindi vitatu.

“Kwa vyovyote vile, mimi nimeshaamua mwaka 2020 nitapumzika. Nitabaki kuwa mwanachama wa Chadema, na nitaendelea kukitumikia chama changu kwa uaminifu lakini nimefika muda ambao napaswa kuwa mpigakura badala ya mchaguliwa,” anasema.

Kabla ya kuwa mbunge, Michael alikuwa diwani wa Kata ya Pasua kwa vipindi viwili mwaka 2005 (Chadema) na mwaka 2010 alichaguliwa pia kuwa meya wa Manispaa ya Moshi.

Kwa sasa Japhary anaongoza jimbo ambalo halijawahi kuondoka mikononi mwa upinzani tangu uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995. Mbunge wa kwanza wa jimbi hilo alikuwa Joseph Mtui kupitia NCCR-Mageuzi.

Pamoja na historia hiyo ya upinzani katika jimbo la Moshi Mjini, kwa sasa kuna kitendawili cha nani atagombea ubunge ndani ya Chadema, ambayo imelishika jimbo hilo kwa muda mrefu, au chama kingine, hasa baada ya Japhary kutangaza kuwa 2020 ndio mwisho wake wa kujihusisha na shughuli za kisiasa.

Hata hivyo Japhary amesema kipindi cha miaka mitano cha ubunge kinamtosha na sasa anahitaji kupumzika siasa na kutulia kuendeleza biashara zake.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad