No title


Mbunge wa Muleba Kusini (CCM), Profesa Anna Tibaijuka amesema uongozi wa Shule ya Sekondari Barbro Johansson Model Girls utarejesha fedha za msaada walizopokea  kutoka kwa mfanyabiashara, James Rugemarila ili aweze kutoka gerezani.

Profesa Tibaijuka amesema hayo kupitia Kituo cha televisheni cha Azam TV.

Amesema uongozi wa shule hiyo umekaa kikao na kuamua kurejesha  fedha hizo walizopokea ili kumsaidia  mtuhumiwa huyo anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kutoka gerezani.

Alipoulizwa kama fedha walizopewa msaada zilikuwa hazijatumika hadi sasa,  Profesa Tibaijuka amesema licha ya fedha hizo kutumika kulipa deni la kujenga bweni la shule lakini zitatafutwa na zitarejeshwa.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Heeeeeh...!! Tibaijuka..Kulikoni,
    Wewe uko Nje, Mshikaji yuko kuleeee.

    unaendelea kumpigia Debe.

    Za shule Hatuzihitaji.
    Tunazitaka zilizo vushwa mipaka mpaka Mashariki ya mbali na Ughaibuni.
    Na zako.

    Msiutumie Ushauri wa Mh. Raisi vibaya na kumtia Doa Mitandaoni kuwa anadai
    pesa za Misaada ya Wasamaria wema(Wapiga Dili / Wahujumu uchumi)
    Zilizo tolewa Mashuleni(Pesa ya Mboga)

    Rugemarila na Seth, Wafilisiwe na Warudise Kisawa sawa Wameiumiza Nchi
    wakishiririkia na kina kama nyinyi na Wale

    ReplyDelete
  2. Tibaijuka..Muleba Oyeee....!!!

    Mama mbona umeamua Kuunguza Picha..!!!

    ReplyDelete
  3. Yana ibuka Maswali juu ya Uhusiano
    wa Mtuhumiwa na msemaji huyu wa Familia.

    Kulikoni..? Diwani upo au umesha kabidhi ofisi. Hili lina kuhusu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad