zimepita tangu msanii aliyekuwa katika lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) Rajab Abdul ’Harmonize’ aondoke na kwenda kuanzisha lebo yake ya Konde Gang, msanii huyo amechaguliwa kuwania katika tuzo kubwa Duniani ya MTVEMA kama Msanii Bora Afrika.
Harmonize ambaye siku za hivi karibuni alitikisa kwa matukio mawili makubwa; kuzindua mgahawa wake unaotembea na kuachia ngoma yake mpya ya Uno, meneja wake amefunguka mambo mengi yanaoendelea kwa sasa kwa msanii huyu hasa kuhusu Tuzo ya MTVEMA anayogombea. Fuatilia mahojiano hapa chini…
Showbiz: Hivi karibuni mlianza kugawa chakula maeneo ya Ilala- Karume kwa kutumia ule mgahawa unaotembea, hii ishu ni kwa Dar tu? Je, itakuwa endelevu?
Meneja: Hiyo ishu itakuwa endelevu, itaendelea kwa miezi sita na itafanyika maeneo mbalimbali nchini, na wala siyo Dar peke yake.
Showbiz: Baada ya kufanikisha Ilala jijini Dar, wapi mpango unahamia?
MENEJA: So far inategemea tumejipanga vipi maana tunaangalia na ratiba ya msanii mwenyewe ipo vipi. Hivyo tutakuwa tukifanya kulingana na muda na ratiba ya Harmonize.
SHOWBIZ: Malengo ni yapi hasa?
Meneja: Ni kuwafikia mashabiki wetu na tunaamini mashabiki zetu wapo nchi nzima, ndiyo maana hii kitu tunataka iwe endelevu.
SHOWBIZ: Umesema hiyo project itaenda kwa miezi sita, unaweza kutuambia labda kila mwezi huwa itagharimu kiasi gani na kwa nini mliamua kufanya hivi? Kwa nini msingefungua mgahawa, watu wakawa wanakuja kula hapo?
MENEJA: Ile ni sadaka, tunalisha kwenye gari kwa hiyo hatuna haja ya kusema itatugharimu kiasi gani, na hatuwezi kufungua mgahawa halafu tukaita watu wote waje kula hapo.
Utaratibu tuliyouanzisha tunaamini utafaa kwa kuwa itakuwa rahisi kufika maeneo mbalimbali na kuwafikia walengwa.
SHOWBIZ: Hili zoezi litakuwa kila baada ya siku ngapi?
MENEJA: Kila wiki.
SHOWBIZ: Harmonize ni msanii aliyefanikiwa kuwania tuzo kubwa za MTVEMA, wewe kama meneja wake unajisikiaje?
MENEJA: Najiona nafanya kitu kikubwa na kazi zetu zinathaminiwa. Sio mimi tu kama meneja, nafikiri Watanzania wote tunajisikia vizuri kwa sababu ukiangalia hii tuzo kwa Afrika Mashariki, msanii ambaye anawakilisha ni Harmonize. Kwa hiyo, naamini Watanzania wote tunajisikia vizuri sana kwa huu uwakilishi.
SHOWBIZ: Tamati ya hizi tuzo ni lini?
MENEJA: Ni Novemba 3, mwaka huu na zitafanyikia katika mji wa Seville (Hispania).
SHOWBIZ: Hivi ni vigezo gani ambavyo waliviangalia mpaka akachaguliwa yeye?
MENEJA: Harmonize kwenye hizo tuzo za MTVEMA anagombea kwenye kipengele cha Msanii Bora Afrika, lakini nafikiri vigezo vyao ambavyo wameweka yeye amekidhi.
Harmonize anafanya muziki wenye test ya Afrobeat, yaani testi yake ni ya Afrika kwa ujumla, siyo Tanzania tu na ndiyo maana amefiti kwenye kipengele hicho. Wanaweza kuwa wameangalia hivyo na vinginevyo.
SHOWBIZ: Una lipi la kuwaambia Watanzania?
MENEJA: Nichukue nafasi hii kuwaomba Watanzania kuendelea kumpigia kura kijana wao kwa wingi kwa sababu siku zimebaki chache halafu hii tuzo ni kitu kikubwa sana kwetu, ukizingatia kwa Afrika Mashariki Harmonize peke yake ndiyo ameweza kutuwakilisha.
Pia waendelee kusapoti kazi za wasanii wetu kwa sababu kwa sasa nadhani muziki Tanzania unafanya vizuri, hivyo tuendelee kuwapa sapoti vijana wetu hasa wale ambao wanafanikiwa kuingia kwenye tuzo mbalimbali za kimataifa. Harmonize anapambana na wasanii kubwa Afrika ambao ni Burna boy, Teni, Nasty C, Prince Kaybee na Toofan.