Meya Boniface Jacob Aelezea Kwa Uchungu Jinsi Anavyozuiwa Airport Asiweze Kusafiri...Kisa Kibali



Mimi Mstahiki Meya Boniface Jacob, Usiku wa Leo Jumamosi kuamkia Jumapili

Nilikuwa Nisafiri kwenda Johanesburg, Nchini South Africa kwa ajiri ya Matembezi binafsi na Dhumuni kuu likuwa nikutanua Mtandao wa Biashara zangu binafsi.

Na ikumbukwe kuwa Safari ya halisi ilipaswa kuwa siku ya Jumamosi Saa 9 na nusu Mchana kwa Mujibu ya Ticket yangu.

Lakini Safari ya kwanza,Jana Jumamosi ilishindikana kwa Sababu nilizopewa ma Maafisa Usalama wa Uwanja wa Ndege na Uhamiaji kuwa Muda usingetosha kunifanyia Mchakato wa Kuniruhusu kupita Uwanjani hapo.

Basi pasipokujua Dhamira yao Ovu,nilikubali kuhairisha Safari na Kugharamia Ticket Mpya.

Basi Leo Usiku Ndege hiyo ilikuwa iondoke Saa 12 asubuhi na Abiria tulipaswa kuanza kugunguliwa Milango(boarding) saa 10 za Usiku.

Ila Kwa Usongo, Saa 9.00. Za Usiku nilikuwa tayari Uwanja wa Ndege Terminal 1 kwa ajili ya Safari.

Basi Leo nikajikuta naangukia Mikononi mwa Maafisa usalama (TISS) na Maafisa Ujamiaji wa Uwanja wa Ndege JKNA,Kisha kupelekwa Kwenye kachumba Maalum kwa mahojiano zaidi.

Huko niliwaeleza kuwa
1.Mimi si Mwajiriwa wa Serikali hivyo sipaswi Kuomba Kibali IKULU.

2.Mimi sikuwa Naenda kuhudhuria Shughuli yeyote kwa Nafasi yangu kama Meya bali Matembezi Binafsi.

3.Sikuwa natumia gharama za Serikali/Halmashauri wala sikugharamiwa na Mfadhili au shirika lolote bali ilikuwa ni pesa kutoka Mfukoni Mwangu.

Pamoja na yote hawakuniachia,
Niliendelea kuwa kizuizini kwa Muda wa Takribani Masaa 3 kuanzia saa 9 Usiku Mpaka Saa 12.

Wakati huo Dakika 10 mdege kuruka, Nasikia nikiitwa kwenye Matangazo ya Ndege kuwa ni "Boniface Jacob is Missing Passenger" niliye jiorodhesha kuwa nipo Uwanjani hapo ila awajui nimepotelea wapi.

Baadae huyo Maafisa Usalama na Uhamiaji na mtu waliyekuwa wanaongea naye wa IKULU aliwaamuru waniache niendelee na Safari,Lakini ilikuwa Imebakia Dakika 10 ndege Kuruka.

Basi Ikawa zamu ya SOUTH AFRICAN AIR WAYS Kuwagomea Maafisa Usalama na Uhamiaji,kwamba Kwa Mujibu wa Taratibu zao walisha niondoa kwenye Orodha ya watu wanaosafiri(Off loading)

Na kweli ndege iliruka nikiwa Uwanjani hapohapo

Leo ni Safari yangu ya Tano narudishiwa Airport na maafisa Usalama na Uhamiaji kwa Kisingizio kuwa Mpaka Kibali Kitoke IKULU.

Safari hii nitaenda tena kuipambania kwa Sababu,nilizotaja hapo Juu,
wala sitokubali Ushauri wa wanaoniambia nipote Njia ya panya Mpaka Msimbiji au Zambia kwanda South Africa,

Sababu Mimi ni Mtu huru siko kifungoni,Wala sina Order ya Mahakama ya Kunizuia Kusafiri kwenda Popote,

Kwa Sababu Mialiko ya kikazi nimeuziwa Minne nikiwa AIR PORT na Moja Ilikuwa Mbaya Sana nilifuatwa kushushwa kutoka Kwenye Ndege,

Na Miaka 3 sasa hata nilipoamua kujishusha Kuomba kibali IKULU Katika Mialiko 20,Sijawahi kupewa Kibali hata 1, Mpaka Leo hii nina Mialiko kama Meya wala sijishughulishi nayo sababu najua Sitoruhusiwa.

Kwa nini na Safari binafsi wanizuie? Nitaitafuta Haki yangu ya kwenda popote! Wala sienda Nje ya nchi kwa kwenda kupandia Ndege Nairobi



Boniface Jacob
Msahiki Meya
Manispaa ya Ubungo
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wewe Bonifasi utapandaje ndege ukiwa Umechemsha Jina na Pasipoti?

    Au unakwenda temino nyingine kusafilia ndege inayo luka temino nyingine unafikili ndege ni gali litasimama na Kupaki upande liendeleee mwendo kasi?

    wewe wa Wapi?

    ReplyDelete
    Replies
    1. tena miradi jimboni inasuasua.
      Asiingie Mitini.

      Delete
    2. hAWA SI NDIO WA KILE CHAMA AMBSCHO M/KITI AMESHA KOSA UHALALI WA KUENDELEA KUSHIKILIA NAFASI.

      SASA INAKUAJE..!!
      AU TUNAFanyaje ..MTORO MWINGINE UGAIBUNI.. MIE SIELEWAGI.. HUYU SAUZI.

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad