Meya Jacob Amshitaki MAKONDA Kwa Rais, "Hatuji Katika Mikutano Kwa Kuogopa Kudhalilishwa Mbele yako"
0
October 27, 2019
Ameandika haya Meya Jacob Katika Ukurasa Wake wa Facebook:
"Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli,leo nimekusikia ukimjibu Makonda kuwa Unatupatia watu wa Ubungo pesa za Kiasi cha Tsh Billioni 1.5 za Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya baada ya yeye binafsi Kukuomba.
Mheshimiwa nakukumbusha wewe na Wasaidizi wako wote kuwa Mwaka huu 2019 Mwezi wa 2 Tarehe 28 Baraza la Manispaa Ubungo lilipitisha Kiasi cha Tsh billioni 84 kuwa bajeti yake ya 2019/2020.
Katika Bajeti hiyo Sisi Manispaa tulitenga kiasi cha Tsh Millioni 250 kwa ajili ya Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya,na tukaiomba serikali kupitia Ruzuku za Miradi ya Maendeleo mnazotushushia mtuletee kiasi cha Tsh Billioni 1.5
July 2019 Bunge likapitisha Bajeti ya TAMISEMI ikiwemo maombi ya pesa zote mbili ,ile ya Wilaya na zile za mapato ya Halmashauri.
Na July hiyohiyo wakati tunafunga Mkutano Mwisho wa Mwaka 2018/2019 katika Baraza la Madiwani nikakushukuru wewe Binafsi na Serikali kuu kutushushia kiasi cha Billioni 3 Pesa za Ujenzi wa Makao Makuu ya Halmashauri,Billioni 1 ya Ujenzi wa kituo cha Afya Kimara Mwisho, na hizo billioni 1.5 za Ujenzi wa Hospitali ya wilaya.
Ila kosa lake Mkuu wa Mkoa nililelile ulilosema wakati Ufunguzi wa Kiwanda Cha Mabomba,ulisema anajishughulisha na Mambo yasiyo ya Msingi na ajui Miradi yoyote katika Mkoa wake,
leo si unaona kakuomba tena kitu kilekile ulichokuwa tayari umeshakifanyia kazi na kukipatia Ufumbuzi,!!
Akiendelea hivyo kuna Siku atakuomba Pesa za Ujenzi wa Flyover Ubungo,Asijue kuwa Mradi upo asilimia 50.
MWISHO
Sisi Viongozi wa Upinzani,Mwanzo tulikuwa tunashiriki Vizuri Mikutano yako tukiamini ni kwa Maslahi ya Taifa,
ila kwa Sasa hatuji tena katika Mikutano yako,ambayo tunajua Mkuu wa Mkoa atashiriki,kwa Sababu amekuwa akitumia Mikutao yako kutudhalilisha Viongozi wenzie mbele yako
Na wewe tunasikitika ujawahi kumkemea hata Mara Moja, kiasi tunafikiria wakati mwingine anatumwa kufanya hivyo au Viongozi wetu Mnafurahia Udhalilishaji huo kwa viongozi wenzie,
Nasisi hatuji kuepusha Shari Mkuu!! "
Boniface Jacob
Mstahiki Meya Ubungo
Source:
Tags