Mfalme wa Thailand amvua vyeo mke wake kwa kutokuwa mwaminifu –
0
October 22, 2019
Mfalme wa Thailand Vajiralongkorn amemvua mkewe vyeo vyake kutokana na “tabia mbaya na kutokuwa mwaminifu kwa ufalme “. Aliteuliwa mwezi Julai , miezi miwili tu baada ya mfalme kumuoa Queen Suthida, mke wake wa nne.
Tangazo rasmi lilisema kuwa Sineenat Wongvajirapakdi alikuwa “mwenye tamaa ” na alijaribu “kujiweka katika hadhi ya malkia “.
“Tabia ya ya mke wa mfalme zilichukuliwa kama ukosefu wa heshima ,” ilisema.
Sineenat, ambaye alikuwa Meja Generali na rubani aliyesomea , muuguzi na mlinzi , alikuwa mtu wa kwanza kutunukiwa cheo cha Mke Mtukufu wa Ufalme.
Malkia Suthida – mwenye umri wa miaka 41- ambaye alikuwa mhudumu wa zamani wa ndege na naibu mkuu wa kikosi cha walinzi wa kifalme – ni mpenzi wa muda mrefu wa is King Vajiralongkorn’s na amekuwa akionekana kuwa nae hadharani kwa miaka mingi.
Kuanguka kwake kutoka cheo cha juu katika ufalme wa Thailand ni mabadilikoya ghafla ya hadhi yake ya juu aliyokuwa nayo ndani ya Ufalme. Kwa miaka mingi mara kwa mara amekuwa akionekana kando ya Mfalme Vajiralongkorn, na aliaminiwa kuwa ndiye mtu aliyekuw
a karibu nae kuliko mtu mwingine.
Hata baada ya kmuoa malkia Suthida, Sineenart alikuwa ndiye mtu aliyeonekana zaidi na kuheshimika katika matukio ya kifalme.
“alionyesha pingamizi na shinikizo kwa njia zote katika kuzuwia uteuzi wa Malkia “kabla ya harusi ya mwezi May.
“Mfalme alimpatia cheo cha mshauri wa ufalme, akiwa na matumaini ya kuondoa msukumo na matatizo ambayo yangeweza kuathiri ufalme ,” lilisema tangazo.
Lakini liliongeza kuwa kuwa Sineenat alionyesha “upinzani dhidi ya mfalme na Malkia ” na kukiuka mamlaka kwa kutoa amri kwa niaba ya kwa niaba ya mfalme.
Tags