Miaka 20 Tangu Mwalimu Nyerere Atutoke je Unazifahamu Nukuu Zake?... Hizi Ni Baadhi

Miaka 20 imetimia tangu kilipotokea kifo cha muasisi wa taifa la Tanzania mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Viongozi mbali mbali wakiongozwa na rais John Pombe Magufuli pamoja na mamia kadhaa ya raia wa nchi hiyo wamejitokeza katika uwanja wa mpira wa Ilulu mjini Lindi katika maadhimisho ya kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru yanayofanyika sambamba na kumbukumbu ya miaka 20 ya kifo cha mwalimu Julius Nyerere.

Mwalimu Julius Nyerere anakumbukwa kwa mambo mengi mazuri aliyoiachia nchi yake Tanzania na Afrika kwa ujumla , ukiwemo umoja na mshikamano na amani miongoni mwa Watanzania pamoja na kuhimiza umoja na mshikamano miongoni mwa watu wa Afrika.

Katika mambo ambayo hayatasahaulika kumuhusu Hayati rais Nyerere ni nukuu zake zilizojaa ujumbe na maudhui hususan zile alizozitoa wakati wa hotuba zake.

1.Hakuna taifa lenye haki ya kufanya maamuzi kwa ajili ya taifa jingine ; hakuna watu kwa ajili ya watu wengine. ( Kutoka 'Ujumbe wa amani wa mwaka mpya ,Tanzania, Januari 1968).
2. Watu wanapaswa kuhusishwa, ili kufikia maendeleo ya kweli. (Julius Kambarage Nyerere (1974)
3. Elimu sio njia ya kuepuka umaskini , ni njia ya kupigana nao.
4. "Umoja hautatufanya kuwa tajiri, lakini unaweza kuwezesha kuiepusha Afrika na watu wa Afrika kutoheshimiwa na kudhalilishwa ". Kutoka katika hotuba aliyoitoa Accra, Ghana, Machi 6, 1997.
5. Katika Tanganyika tunaamini kuwa ni waovu , watu wasiomuamini Mungu wanaoweza kuifanya rangi ya mwili ya binadamu kuwa kigezo cha kumpa haki zake za kiraia ". Akizungumza na Gavana wa Uingereza , General Richard Gordon Turnbull, kabla ya kuchukua kiti cha uwaziri mkuu mnamo mwaka 1960.
6. "Demokrasi sio chupa ya Coca-Cola ambayo unaweza kuiagiza. Demokrasi inapaswa kuendelezwa kulingana na nchi yenyewe ". Juni 1991 mjini Rio De Janeiro, Brazil.
7. Hatuwezi kuwa na matumaini ya kutatua matatizo yetu kwa kujifanya kuwa hayapo.
8. Itakuwa yote ni makosa , na si jambo la muhimu , kuhisi kuwa lazima tusubiri hadi viongozi wafe ndio tuanze kuwakosoa " JK Nyerere.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad