Mjane aipongeza Serikali kwa kumsaidia kupata Ng'ombe zake zilizotapeliwa

Mama Mjane, Kundi Machiye akiwa katika hali ya furaha baada ya mifugo yake kuokolewa na Takukuru baada ya Afisa Mtendaji, Jaston Mpigauzi kutaka kuwauza ili apate Milioni 4.6 za faini akidai watoto wa mama huyo walimpiga na kumjeruhi mwalimu wa chekechea
Na. Baraka Messa, Songwe

Mama mjane Kundi Machiye (50) ameipongeza Serikali ya awamu ya tano chini ya Dkt, Rais John Magufuli baada ya Takukuru wilayani Songwe mkoani Songwe kumsaidia kuokoa Ng'ombe 25 ambazo zilitolewa kama rushwa kwa mtendaji wa kijiji cha Kapalala Jaston Mpigauzi  ili aweze kuwaachia watoto wa mama huyo waliotuhumiwa kumpiga mwalimu wa shule ya Chekechea kibaoni.


Mchuuzi,Ibrahim Yassin aliyenunua Ng'ombe hao kwa Afisa Mtendaji Kata ya Kapalala, Jaston Mpigauzi ambao tayari Takukuru wamewaokoa na mtendaji huyo anashikiliwa yupo mbioni kuchukuliwa hatua za kisheria
Kundi Machiye Dubala ambaye ni  mama mjane alisema kuwa  anaishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kutenda haki ambapo yeye amefanikiwa kupata mifugo yake 25 ambayo tayari ilikuwa mnadani kwa ajiri ya kuuzwa akisaidiwa na TAKUKURU wilaya ya Songwe.

Alisema siku ya tarehe 17 septemba 2019 akiwa safarini Ikonda alipata taarifa za watoto wake kupigwa na kuumizwa na afisa mtendaji wa kijiji cha kapalala huku ng'ombe zake 25 zikichuliwa na mtendaji kwa kudai kuwa vijana hao wameshindwa kulipa fedha kias cha shilingi 4,650,000 baada ya kudaiwa kumpiga mwalimu.

"Nilipiwa simu na afisa mtendaji Mpigauzi kuwa niende haraka niwapeleke wanangu hospitali , huku fedha ambazo aliomba rushwa akilipwa na mchuuzi wa ng'ombe kijijin hapa JilatuMasuluzu ambaye alichukua ng'ombe zangu na kupeleka mnadani" alisema Kundi.

Alisema aliamua kwenda TAKUKURU wilaya ya Songwe ambapo alipewa ushirikiano mzuri na kufanikiwa kupata mifugo yake yote ikiwa mnadani kwa ajili ya kuuzwa na mchuuzi huyo wa kijiji cha Kapalala.

Akizungumzia tukioa lililotokea septemba 16 mwaka huu 2019  mkuu wa Takukuru Mkoa wa Songwe Damas Suta alisema  Afisa mtendaji Jaston Mpigauzi aliomba rushwa ya shilingi 4,650,000 ili aweze kuwaachia na kutowafikisha kwenye vyombo vya sheria ndugu wawili Mpemba Lusambala Jiloya pamoja na Jihumbi Lusambala Jiloya waliokuwa wamekamatwa na afisa Mtendaji huyo kwa kosa la kumshambulia mwalimu wa shule ya Chekechea Kibaoni.

Alisema baada ya watoto hao wawili kukosa fedha hizo za rushwa ambazo aliomba afisa mtendaji , fedha hizo zilitolewa na mchuuzi ampapo mtendaji aliwaagiza ndugu hao wawili aliokuwa amewakamata kwenda kumpatia mchuuzi huyo jumla ya ng'ombe 25  kama fidia ya fedha Tshilingi 4,650,000 alizotoa.

Ambapo Mkuu wa TAKUKURU anadai kuwa ng'ombe hao 25 kama wangeweza uzwa kwa bei ya soko gharama ya  shilingi laki nne (400,000) kila mmoja mmiliki angeweza kupata Tsh 10,000,000/=

Suta alisema TAKUKURU wilayani Songwe baada ya kupata taarifa ilifanya ufuatiliaji na  kufanikiwa kurudishwa kwa Ng'ombe wote 25 aliokabidhiwa mchuuzi huyo kama fidia ya hongo iliyotoka kwa afisa mtendaji wa kijiji.

aliongeza kuwa baada ya kufanikisha kurudisha mifugo hiyo TAKUKURU wataujulisha umma hatua zitakazochukuliwa kwa mtendaji huyo na waliohusika ili kuwa fundisho kwa viongozi wengine wenye tabia kama hizo ambazo ni kinyume na sheria za nchi.

Awali Mpigauzi alikua afisa mtendaji wa kata ya Ng’wala ambapo alikuwa na matukio mfululizo ya kuwatoza faini kandamizi wafugaji ambapo pia fedha hizo zilidaiwa kutopelekwa hofisi za halmashauri.

Siku za hivi karibuni katika kikao kilichoitishwa na viongozi wa wafugaji wa kitaifa wakiongozwa na Mwenyekiti wao George Bajuta iliibuka tuhuma ikimhusu mtendaji huyo kuingia kwenye nyumba ya mmoja wa wafugaji akiwa na panga lililokolezwa moto ambapo ilidaiwa alimchoma mgongoni mfugaji baada ya kugoma kutoa fedha.

Taarifa za mtendaji huyo kuwatoza faini kandamizi wafugaji zilifika ofisi za wilaya ya Songwe lakini ilielezwa kuwa badala ya kuchukuliwa hatua mtendaji huyo alihamishiwa kituo cha kazi kutoka Ng’wala akahamishiwa kata ya Kapalala hali iliyopelekea wafugaji kuendelea kupatashida kutokana na mtendaji huyo.

Kaimu TAKUKURU Wilaya ya Songwe Robert Kahimba alisema baada ya kukaa muda mfupi wilayani humo amegundua kuwa kuna baadhi ya viongozi wasio waadilifu wilayani humo ambao wamekuwa wakikiuka na kupokea rushwa kwa wafugaji jambo ambalo ni kutowatendea haki wafugaji na kukiuka sheria za nchi hii ambayo ina utawala wa kisheria.

"Wafugaji wengi wamekuwa wakiogopa pindi wanapo ambiwa kuwa watafikishwa kwenye vyombo vya sheria hata bila kosa, TAKUKURU hivi sasa tupo wilayani Songwe hivyo wananchi wote waripoti taarifa zozote ambazo zinawanyima au kuwataka kutoa rushwa," alisema Kahimba.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad