Leo October 3, 2019 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila, awatandika bakora wanafunzi zaidi ya 13 wa shule ya Sekondari ya Kiwanja iliyopo wilayani Chunya baada ya kubaini wanamiliki simu wakiwa shuleni.
Chalamila alichukua uamuzi huo Mara baada ya Kutembelea shuleni hapo na kupokea Taarifa ya Shule kutoka kwa Mkuu wa shule hiyo, kuwa kuna baadhi ya wanafunzi wanamiliki Simu kitu ambacho ni kinyume na Taratibu za Shuleni hapo.
Mbona tatizo Hilo lingetatulika tu katika ngazi ya shule kama ilivyo katika matatizo mengine kama kuchelewa shuleni au kufika darasani nk. Wala halikuhitaji mkuu wa mkoa. Mkuu wa shule vipi?! Mkuu wa mkoa vipi tena!? Bora serikali irudishe utaratibu wa kutoa semina elekezi kwa wakuu husika kabla ya kuanza kazi.
ReplyDelete