DC, DED Nachingwea Matatani…Rais Atoa Onyo


 Dar es Salaam. Rais wa Tanzania John Magufuli amewabana Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea (DC) Rukia Muwango na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bakari B Bakari baada ya wananchi kulalamikia ucheleweshwaji wa miradi ya maendeleo.

Tukio hilo limetokea leo Jumatano Oktoba 16, 2019 wakati Rais akihutubia wananchi katika wilaya ya Nachingwea ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika mkoa wa Lindi.

Baada ya hotuba za viongozi mbalimbali, Rais alimuomba Mwenyekiti wa CCM, Mzee Hashim Mkanjauka aeleze matatizo yote yanayowakabili wakazi wa Nachingwea.

Mkanjauka alianza kuelezea miradi ya maendeleo iliyokwama hali iliyowafanya wananchi waibuke kwa shangwe na hivyo kumfanya Rais atake kujua Zaidi kero hizo.

“Viongozi wetu siyo wakweli, miradi wilaya ya Nachingwea vijijini haitekelezeki, stendi ya wajasiriamali hakuna, soko halina kitu mkandarasi waliyempa hajamaliza, redio imenunuliwa na kufungwa kwa fedha za wananchi zaidi ya Sh100 milioni lakini haifanyi kazi. Maji yamekuja na mwenge yameondoka na mwenge Nachingwea ni wilaya kongwe,” amesema Mzee Mkanjauka.

Baada ya maelezo hayo Rais alimuita Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo akimtaka atoe majibu ya kwanini miradi hiyo inasuasua na mingine imesimama kabisa

Mwananchi
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad