Msafara wa MAGARI ya Kijeshi ya Marekani Wakiondoka Syria Kuhamia Iraq

Msafara wa magari ya kijeshi ya Marekani umeonekana ukiondoka kaskazini mwa Syria
Vikosi vyote vya Marekani vinavyoondoka kaskazini mwa Syria vinatarajiwa kuhamia magharibi mwa Iraq, waziri wa ulinzi Mark Esper, amethibitisha.

BW. Esper amewaambia wanahabari kuwa, chini ya mpango wa sasa karibu wanajeshi 1,000 watapelekwa Iraq kusaidia katika juhudi za kuzuia kurejea upya kwa kundi la Islamic State (IS).

Rais Donald Trump amewahi kuahidi kuwarejesha nyumbani wanajeshi wa Marekani.

Rais Magufuli awaapisha maafisa wapya serikalini
Eliud Kipchoge atuzwa shujaa wa taifa
Wavishwa maboxi kufanya mtihani
Kuondoka kwa vikosi vya Marekani kaskazini mwa Syria kulitoa nafasi kwa Uturuki kuanzisha oparesheni ya kijeshi dhidi ya wapiganaji wa Kikurdi.

Pande zote mbili zimekuwa zikilaumiana kwa kukiuka mkataba wa kusitisha mapigano ulioongozwa Marekani.

Ankara inawachukulia wanamgambo walijumuishwa katika vikosi vya Kikurdi ni magaidi, hatua iliyoifanya kubuni "eneo salama" ndani ya Syria.


Maelfu ya watu wametoroka makazi ya katika eneo la kaskazini mwa Syria tangu Uturuki ilipoanzisha opareshani dhidi ya wapiganaji wa Kikurdi
Siku ya Jumapili, Uturuki ilisema kuwa mmoja wa wanajeshi wake ameuawa na mwingine kujeruhiwa wakati wakikabiliana na wapiganaji wa Kikurdi karibi na mji wa Syria wa Tal Abyad.

Vikosi vya Kikurdi viliwahi kuilaumu Uturuki kwa kuvikataza kuwahamisha watu wake kutoka mji wa mpakani.

Huku hayo yakijiri, Spika wa bunge la Marekani Nancy Pelosi amewasili nchini Jordan kufanya mazungumzo na Mfalme Abdullah.

Bi Pelosi, ambaye ameandamana na wanasiasa wa ngazi ya juu wa Marekani, amekosoa vikali hatua ya rais Donald Trump kuwaondoa wanajeshi wa nchi hiyo kaskazini mwa Syria.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad