Mtoto mchanga wa kike amepatikana akiwa amezikwa hai katika kaburi la kina kifupi kaskazini mwa India, mkuu wa polisi afichua kisa hicho.
Abhinandan Singh amewaambia wanahabari kuwa mtoto huyo alipatikana na mwanakijiji aliyekuwa ameenda kumzika mtoto wake aliyefariki baada ya kuzaliwa.
Mtoto huyo aliyekuwa amewekwa ndani ya chunguu na kuzikwa katika shimo la futi tatu, amekimbizwa hospitali ambako anapokea matibabu.
"Tunajaribu kutafuta wazazi wa mtoto huyo kwani tunashuku huenda hatua hiyo ilifikiwa kutokana na idhini yao," Bw. Singh aliwaambia wanahabari katika jimbo la Uttar Pradesh.
Kwa mujibu wa mkuu huyo wa polisi, mwanakijiji mmoja wlimpata mtoto huyo alipokuwa akifukua kaburi la kumzika mwanawe aliyefariki baada ya kuzaliwa.
"Walipokuwa wanaendelea na shughuli ya uchimbaji kaburi kijiko cha kutoa mchanga katika shimo liligonga chungu kilichokuwa kimezikwa fiti tatu. walilopokitoa walipata ndani kuna mtoto," Bw Singh alieleza.
"Polisi walimpeleka mtoto huyo katika hospitali iliyo karibu ambako anaendelea kupokea matibabu."
Suala La kijinsia nchini India linatajwa kuwa katika hali mbaya zaidi duniani.
Wanawake mara nyingi hubaguliwa katika jamii hukiu watoto wa kike wakichukuliwa kama mzigo wa kiuchumi, hasa katika jamii masikini.
Wanaharakati wa kutetea usawa wa kijinsia wanasema watoto wa kiume wanapendelewa zaidi kuliko wa kike.
Japo mimba za watoto wakike mara nchini hutolewa baada ya wazazi kubaini jinsia ya mtoto kupitia kiliniki zilizopigwa marufuku, visa vya watoto wa kike kuawa baada ya kuzaliwa vimekuwa vikiripotiwa mara kwa mara.