Muna: Talaka Imenifanya Nianze Kunenepa


WAKATI wengine wakipewa talaka hupungua mwili kwa stress! Kwa msanii wa filamu Bongo ambaye pia ni mjasiriamali, Rose Alphonce ‘Muna’ ni tofauti kwani tangu aipokee talaka yake mkononi, ameona hata afya ya mwili wake imeanza kubadilika.

Akizungumza na Za Motomoto ya Risasi, Muna alisema mwili wake umeanza kunenepa kwa sababu hata akila chakula, kinapita bila shida yoyote wala mawazo maana talaka ilikuwa inamfanya anakosa amani na furaha ya moyo.

“Yaani ndani ya wiki moja tu mwili umeshabadilika, kweli nilikuwa kwenye kifungo kikubwa sana maana chochote ninachokula kwasasa kinapita vizuri sana na watu watashangaa mabadiliko yangu kwa kuwa walikuwa hawajui nini kinanitesa,” alisema Muna.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad