Mvua yakwamisha Safari za Treni


Shirika la Reli nchini (TRC), limesitisha huduma za usafirishaji wa mizigo katika ukanda wa kaskazini mikoa ya Kilimanjaro na Tanga kuanzia Oktoba 26, 2019 kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Shirika hilo limeomba radhi katika taarifa waliyoitoa inatoeleza kuwa kutikana na mvua kubwa zinazazoendelea kunyesha katika ukanda huo na kusababisha mito ya pangani (Ruvu na Rwengara) kujaa maji ambayo yameelekea relini.

Shirika hilo limesema linaendelea na jitihada za ukarabati na litatoa taarifa njia itakapotengamaa na kurejea kwa usafiri kama awali.

Hadi sasa maji hayo yamesababisha uharibifu wa miundombinu, yakiwemo madaraja ambapo sehemu zilizoathirika ni Muheza, Korogwe na Mombo kipande kilichoharibika madaraja mawili, na Wami Makinyumbi kipande ambacho kimeharibika makaravati manne.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad