Mwananmke ajiua baada ya kutaniwa na mume wake kuwa ana ngozi nyeusi
0
October 31, 2019
Mwanamke mmoja nchini India mwenye miaka 21 anadaiwa kujiua kutokana na kudhalilishwa na mumewe kwa sababu ya ”rangi nyeusi” ya ngozi yake.
Polisi wa jimbo la Rajasthan wamefungua kesi dhidi ya mume wa mwanamke huyo baada ya baba wa marehemu kumshutumu mume kuwa chanzo cha kifo cha binti yake.
Polisi kutoka nchini India kuwa mwanaume huyo hajakamatwa. Na mume akiwa bado kutoa taarifa kuhusu shutuma dhidi yake.
Raia wengi wa India wana mtazamo kuwa rangi nyeupe ni watu wa tabaka la juu kuliko wahindi weusi.
Baba wa mwanamke huyo aliiambia polisi kuwa mume wa binti yake mara kwa mara alikuwa ”akimdhalilisha kwa sababu ya weusi wa ngozi yake”, vitendo ambavyo vilimfanya ayakatishe maisha yake.
Hii si mara ya kwanza kwa vitendo vya dhihaka dhidi ya wanawake wa India wenye rangi nyeusi kutokea na kusababisha vifo.
Mwanamke mmoja mwenye miaka 29 alijiua mwaka 2014 baada ya mumewe kudhihaki rangi ya ngozi yake, polisi wameeleza.
Na mwaka 2018, binti wa miaka 14 alijiua baada ya wanafunzi wenzake kumzomea kuwa ana ”muonekano mbaya” kwa sababu ya rangi ”nyeusi ” ya ngozi yake.
Picha ya mikono ya bibi harusiMikono ya bibi harusi wa nchini India
Tukio hili la kutisha kwa mara nyingine linaonyesha namna gani kuhusudu sana rangi nyeupe/angavu ya ngozi kumesababisha hatari nchini India.
Tangu watoto wadogo, wasichana wenye rangi nyeusi huitwa majina ya dharau. hudhalilishwa shuleni, kwenye viwanja vya michezo hata majumbani, huku wakifananishwa na ndugu wengine ambao si weusi.
Katika masuala ya kujiandaa na ndoa safu za magazeti husisitiza mara zote kwa kuonyesha maharusi wa kike wakiwa na rangi angavu, nyupe au kahawia, lakini si rangi inayokaribia nyeusi.
Vyombo vya habari mashuhuri huonyesha picha za wana mitindo na wacheza filamu wenye rangi nyeupe.
Hali inayofanya wanawake wenye rangi nyeusi kujiona hawafai, au wasio na mvuto wowote.
Kwa mujibu wa BBC. Sheria zinazuia matangazo kuonyesha watu wenye ngozi nyeusi kama wasio na furaha au wasio na mvuta, na miaka ya hivi karibuni matangazo yamekuwa yakiwasilishwa kwa namna nyingine ya kibunifu ambayo mwisho wa siku ujumbe huwa ni ule ule kuwa weupe ni mzuri.
Miaka michache iliyopita, kulikuwa na kampeni za kupinga watu kuwa na sherehe za watu wenye ngozi nyeusi, lakini ni wazi kuwa jitihada zaidi zinapaswa kuongezwa kufikisha ujumbe huu.
Mpaka hapo hatua zitakapochukuliwa kukomesha vitendo hivi, vitendo na tabaia za kibaguzi zitaendelea kugharimu maisha ya watu
Tags