Mwanaume Afunga Ndoa na Maiti Banda ya Mkewe Kufariki na Kansa ya Matiti


Mapenzi ya kweli ! Katika hali isiyo ya kawaida jamaa pichani kwa jina la Xiu Shinan(35) siku ya mazishi amefunga ndoa na maiti ya mpenzi wake Yang Liu(34) aliyefariki kwa kansa ya matiti. Amesema hiyo ndio heshima aliyoamua kumpa mpenzi wake huyo kwani ilikuwa ndoto yake siku moja aje kuitwa bibi harusi. Siku ya mazishi jamaa alienda nunua gauni la harusi ambalo lilivishwa maiti ya mdada huyo. Tukio Hilo limehudhuriwa na ndugu wa familia zote pamoja na marafiki

Wawili hao waliokaa Kwenye mahusiano Kwa miaka 12 walisoma chuo kikuu darasa moja. Mwaka 2013 walipoanza taratibu za ndoa Yang alianza kulalamikia kuumwa kifuani, walisitisha kwanza ndoa Ili  kushughulikia matibabu ya Yang baada ya kugundulika na ugonjwa huo 2014.

Mwaka 2017 hali ya Mdada huyo ikaanza kutengamaa wakaanza tena mishe za kufunga ndoa lakini mwaka mmoja baadaye ugonjwa ukarudi ambapo hali ikawa Mbaya zaidi na sasa amefariki 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad