Mwinyi Zahera afunguka kuhusu Molinga



Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera, amesema kuwa mshambuliaji wake, David Molinga bado hajaanza kazi na kwamba ana vitu vingi ambavyo hajaonyesha uwanjani hivyo mashabiki wasubiri.

Molinga ni mshambuliaji mpya wa Yanga amejiunga kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea timu ya AC Lega ya DR Congo akichukua mikoba ya Heritier Makambo aliyetimkia AC Horoya ya Guinea.

Mechi ya mwisho dhidi ya Polisi Tanzania, Molinga aliiokoa Yanga isiaibishwe nyumbani pale Uwanja wa Uhuru kwa kufanikiwa kuisawazishia kwa kufunga mabao mawili baada ya Yanga kuwa nyuma kwa mabao 3-1.

Zahera alisema kuwa, hana mashaka na uwezo wa mchezaji wake ndiyo maana akamleta ndani ya kikosi hicho. “Molinga ni mshambuliaji aliyekamilika akiwa ndani ya uwanja kufuatana na vile ambavyo ninamjua namna anavyofanya akiwa uwanjani kwani sijamjua jana ni siku nyingi.

“Ligi ina michezo mingi naye atacheza michezo mingi zaidi ili afunge zaidi kwani najua akiendelea kucheza na wenzake atajiongezea hali ya kujiamini na kupata nafasi ya kuelewana na wachezaji wenzake,” alisema Zahera.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad