Mwinyi Zahera Apewa Mtihani Yanga
0
October 21, 2019
Kikosi cha Yanga juzi asubuhi kilitua jijini Mwanza tayari kwa mechi zake mbili jijini humo katika Uwanja wa CCM Kirumba ambazo ni mtihani wa aina yake.
Mechi hizo ni ile ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbao FC itakayochezwa Jumanne ijayo, lakini pia ile ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Pyramids ya Misri itakayopigwa Oktoba 27.
Katika kuelekea mechi hizo, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela ameliambia Spoti Xtra kuwa maandalizi yao kwa upande uongozi yamekamilika, kazi pekee iliyobakia ni benchi la ufundi la timu hiyo kuhakikisha wanapata ushindi.
Alisema kwa upande wa uongozi wamefanya kila kitu ikiwa ni pamoja na zawadi mbalimbali ambazo watawapatia wachezaji wao pindi watakapofanya vizuri katika mechi hizo.
Kwa upande wake kocha Mwinyi Zahera ameliambia gazeti hili kuwa; “Kila kitu nilichokuwa nimemwachia msaidizi wangu, Noel Mwandila wakati nilipokuwa katika majukumu ya timu ya taifa nimekuta kipo sawa.
“Kwa hiyo ni matumaini yetu kuwa tutafanya vizuri katika mechi hizo. Wachezaji wote wapo sawa isipokuwa Banka (Mohammed Issa) pamoja Issa Bigirimana ambao ni majeruhi na tutawakosa katika mechi hizo mbili,” alisema Zahera.
Tags