Ndege ya Abiria Yaanguka katika Uwanja wa ndege wa Wilson jijini Nairobi Kenya


Ndege moja inayoendeshwa na kampuni ya Silverstone Air imeanguka katika uwanja wa ndege wa Wilson katika mji mkuu wa Nairobi nchini Kenya.

Walioshuhudia wanasema kwamba ndege hiyo ilipoteza mwelekeo wakati ilipokuwa ikipaa kuelekea Mombasa Ijumaa Alfajiri.

Picha kutoka eneo la mkasa zinaonyesha kwamba ndege hiyo ilianguka katika kichaka , ikigonga miti na kuvunja mojawapo ya mbawa zake kabla ya kuangukia ubavu mmoja.

Abiria mmoja ambaye alikuwa ameabiri ndege hiyo aliambia chombo cha habari cha Nation kwamba walikuwa bado hawajafika angani wakati rubani alipogundua matatizo.

Hakuna ripoti za moja kwa moja kuhusu majeruhi lakini abiria wengi walipatwa na mshtuko baada ya kunusurika kifo.


Ndege yaanguka katika uwanja wa Wilson Nairobi Kenya
Vikosi vya kukabiliana na dharura katika uwanja huo wa ndege viliwaondosha abiria katika ndege hiyo na kuwakimbiza katika hospitali mbalimbali ili kufanyiwa vipimo.

Shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya Red Cross liliripoti kwamba ndege hiyo aina ya 5Y-IZO ilikumbwa na matatizo ya kiufundi wakati ilipokuwa ikipaa.

Wazima moto waliwasili katika eneo hilo katika muda uliofaa , waliimwagia maji ndege hiyo ili kujaribu kuzuia moto kuwaka.

Katika taarifa fupi katika mtandao wake wa twitter kampuni ya Silvertsone Air ilithibitisha kutkea kwa tatizo hilo , ikisema kwamba ndege hiyo ilikuwa ikiendeshwa kutoka Wilson, kuelekea , Lamu na Mombasa.

Abiria wote na wafanyakazi a ndege wametolewa na ka sasa tunashirikiana na mamlaka husika kuchungza hali, ilisema taafira.

Mamlaka ya ndege nchini Kenya KAA na wasimamizi wa Uwanja wa ndege wa Wilson hawajatoa tamko lolote kuhusu kisa hicho.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad