SEPTEMBA 28, mwaka huu ilikuwa siku ya historia kwa mashoga maarufu nchini Afrika Kusini, Somizi Mhlongo (mtangazaji na msanii) na Mohale Motaung (mwanachuo na mjasiriamali) walioamua kufunga ndoa ambayo imeonekana kulaaniwa na wengi wanaojali maadili.
Ndoa hiyo baadaye ilifuatiwa na sherehe ya kimila iliyofanyika kwenye nyumba ya familia iliyopo Motaung jijini Johannesburg.
Wakati Somizi na Mohale wanaanza uhusiano wao mwaka 2017 lilikuwa kama jambo la kushangaza na lililoonekana machoni pa watu kuwa si jambo la kweli huku wengine wakisema Mungu aepushie mbali laana hiyo.
Hata hivyo mapenzi ya mashoga hao yalipokolea, walishindwa kuficha hisia zao mbele ya jamii ambapo walianza kujiachia ingawa mara kadhaa walikuwa wakikanusha kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja.
Wakifafanua katika jumbe zao kwenye kurasa zao za Instagram mwaka jana, wawili hao walikiri kuwa walianza uhusiano wao mwaka 2017.
Somizi ambaye alizaliwa Desemba 23, 1972, alikua na kulelewa kama watoto wengine wa kiume lakini alivyojifunza ushoga hajafafanua mahali popote licha ya kukiri mara kadhaa kuwa kuna wakati alishindwa kujitambua jinsia yake.
“Nilipokuwa na miaka 7, nilikwenda kuanza shule lakini baada ya miezi sita sikuwa na hamu tena ya kusoma, nilipenda kuishi na wazazi wangu,” alisema Somizi alipokuwa akihojiwa na Kituo cha Televisheni cha eTV mwaka 2014.
Somizi katika nchi ya Afrika Kusini si ‘mtu mdogo’ kwani ni muigizaji mwenye heshima kubwa ambapo mwaka 1987 alitikisa na Muvi yake ya Scavengers na miaka michache baadaye alikuwa miongoni mwa mastaa walioshiriki kwenye filamu ya Sarafina sambamba na staa wengine kama Whoopi Goldberg, Miriam Makeba na Leleti Khumalo.
Pengine umaarufu wake ndiyo uliokuwa ukiwafanya watu wengi wasite kuamini kama anajihusisha na vitendo hivyo vichafu kwani mbali na uigizaji ni mwanamuziki.
Ushoga wa Somizi haukuwachanganya watu tu lakini hata wazazi wake kwani mbali na kujihusisha nao lakini alionekana kuwa na uhusiano na wasichana wengine jambo ambalo wazazi wake hawakuwa na hata tone moja la wasiwasi kuhusu jinsia yake.
Somizi mbali na ‘kudeti’ na wasichana wengi alikuwa na uhusiano wa wazi na mwigizaji maarufu wa kike, Palesa Madisakwane.
Palesa alifanikiwa kumzalia Somizi mtoto wa kike aliyempa jina la Bahumi lakini ndiyo huyo ambaye Septemba 28, amefunga ndoa na shoga mwenzake, Mohale.
Hata hivyo, kama yalivyo mapenzi mengine hali ya kupanda na kushuka ni jambo la kawaida kwani uhusiano wa Somizi na Mohale mapema mwaka huu uliripotiwa kuvunjika.
Wapenzi hao wa kiume kila mmoja alimfuta urafiki mwenzake katika ukurasa wake wa Instagram na kila mmoja kukoma kuposti picha ya mwenzake.
Ishara hiyo iliwafanya baadhi ya watu nchini Afrika Kusini kuona kama ‘mchezo mchafu’ ulikuwa umeishia hapo, lakini haikuwa hivyo.
Kitu cha kwanza alichokuja kuibuka nacho Somizi ni nia yake ya kuifanya jamii kujua wazi kuwa ameamua kuwa shoga na yuko tayari kwa ndoa mbali na wengi kutopendezwa kabisa na vitendo hivyo vinavyopingwa na watu wengi duniani.
Katika kuonesha kuwa dunia inaelekea kubaya, Mohale naye ambaye amezaliwa Julai 9, 1994 katika eneo la Kibler Park, Johannesburg alionekana kutojali, badala yake alionesha mapenzi yake kwa Somizi.
Ndoa ya wawili hao iliyoshangaza Afrika iliwakera wengi walioona picha zao mitandaoni na kusema kuwa, walichokifanya kinaashiria mwisho wa dunia.
“Hili kwa nchi nyingine lisingewezekana, bakora zingetembea na hii ni ishara ya mwisho wa dunia,” aliandika mtandaoni Joackim Super.
Katika kuonesha kuwa dunia inaelekea kubaya, Mohale naye ambaye amezaliwa Julai 9, 1994 katika eneo la Kibler Park, Johannesburg alionekana kutojali, badala yake alionesha mapenzi yake kwa Somizi.
Ndoa ya wawili hao iliyoshangaza Afrika iliwakera wengi walioona picha zao mitandaoni na kusema kuwa, walichokifanya kinaashiria mwisho wa dunia.
“Hili kwa nchi nyingine lisingewezekana, bakora zingetembea na hii ni ishara ya mwisho wa dunia,” aliandika mtandaoni Joackim Super.