Hili jambo limeniuma sana tena sana, wanawake wengi wanaonewa na waume zao bila kusema popote wakijua ndio kuvumilia kumbe hawajui wanajiua pasipo kujua inaniuma sana.
Nimeongea nawanawake zaidi ya 20 walio wengi hawana raha ya ndoa au tuseme tuu ya maisha wanasema wanavumilia huku miaka inaenda wakiwa ndani ya mateso makali, Kama kulea familia wenyewe bila kusaidiwa na baba hata senti, kufungiwa nje bila huruma yani kufukuzwa, kutukanwa na kudharauliwa, kupigwapigwa hivyo hata kuachiwa ulemavu, kubebeshwa mzigo wa kulea watoto wenyewe au kutelekezewa watoto mwanaume akapotea kabisa nyumbani baada ya miaka kumi hadi ishirini ndio anarudi na watoto wanamfurahia bila mama kufanya lolote, wanaume 98% kutokuwa waaminifu ndani ya ndoa zao, kuambukizwa magonjwa ya zinaa na ukimwi, na kugeuzwa kuwa punda wake bila huruma, kwakweli hili jambo limeniuma sana wanaume walio wengi ni mashetani wanaigiza kuwa binadamu hivyo kupelekea wana wake kufa haraka.
Wanawake embu zindukeni kuna maisha zaidi ya ndoa, msikubali kufa mapema kisa neno ndoa yapo maisha zaidi ya ndoa bana msikubali kunyanyaswa hata kidogo yapo maisha bila mume na yenye amani msikubali utumwa nikujitengenezea kifo chakujitakia.
Hii ni rai kwa wanawake wote walio ndani ya ndoa nawale wanaotarajia kujiunga na ndoa, ndoa sio mateso, ndoa sio msalaba, ndoa sio uvumilivu wala ndoa sio lazima.