Ofisi ya Kikwete Yafafanua Hotuba Yake
0
October 11, 2019
OFISI ya Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, imeeleza masikitiko yake kuhusu upotoshaji unaofanywa na baadhi ya watu kuhusu hotuba aliyoitoa kwenye Kongamano la Kumbukizi ya Miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere
Imesema kuwa mada ya Kongamano hilo ilikuwa ‘Urithi wa Mwalimu Nyerere katika Uongozi, Maadili, Umoja na Amani katika Ujenzi wa Taifa’ na Kikwete alieleza kwa namna alivyomfahamu Mwalimu Nyerere kulingana na mada hiyo
Ofisi hiyo imesema Kikwete ameshangazwa na kusikitishwa kwa kujitokeza watu wanaopotosha ukweli kuhusu maneno yake na kuwepo wanaojaribu kumwekea maneno wakidai eti alikuwa anawasema baadhi ya viongozi waliopo sasa.
Aidha, ofisi imeeleza kuwa hakufanya ulinganifu kati ya Mwalimu na marais waliofuata baada yake, waliostaafu na waliopo sasa pia hakutaja jina la mtu yeyote, hivyo kusikia kuwa alisema mtu ni jambo linalosikitisha na ni uzandiki, fitna na uchonganishi
Mwisho, Kikwete amesema alitegemea watu wamkosoe kwa aliyoyasema na si kumsingizia na pia amewataka watu wenye maoni yao wawe wajasiri na kuyasema na si kujificha katika kivuli cha hotuba yake.
Tags