Padri wa Kanisa Katolriki Aliyepotea siku saba Mwili Wake Umekutwa Umefukiwa


Padri wa kanisa katoliki nchini Kenya aliyekuwa ametoweka kwa siku saba baada ya kutekwa, mwili wake umepatikana ukiwa umefukiwa kwenye kingo za mto.

Kwamujibu wa taarifa zilizotolewa na jeshi la polisi, imeelezwa kuwa mwili wa Padri Michael Maingi Kyengo (43), ulipatikana baada ya moja ya watuhumiwa kuwaelekeza polisi siku ya jumanne, aneo walilo fukia mwili huo.


Imeelezwa kuwa Padri huyo alitoweka kutoka kanisa la Thatha lililopo Machakos Oktoba 8 mwaka huu, na imeelezwa kuwa kwa mara ya mwisho aliondoka hapo na gari lake lakini hakurejea tena.

Mwili wake umechukuliwa na jeshi la Polisi na kupelekwa hospitali kwaajili ya kufanyiwa uchunguzi zaidi.

Kamanda wa polisi, Daniel Rukanga, amesema ” Tunataka kufanya uchunguzi kwenye mwili wake ili ukweli ubainike, na tutatafuta chanzo cha mauaji haya kwa kuendelea na uchunguzi kwa watuhumiwa wote walio husishwa na mauaji ya kiongozi huyu”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad