Papa Francis amtangaza kadinari Newman kuwa mtakatifu mpya


Kadinari John Henry Newman ametangazwa kuwa mtakatifu na kanisa katoliki, katika maadhimisho ya misa iliyoongozwa na papa Francis hii leo huko Rome, Italia. Misa ya wazi ilihudhuriwa na maelfu ya watu waliokuja kwenye hija.



Kadinari Newman, ambaye alifariki huko Birmingham mwaka 1890, ni muingereza wa kwanza kutangazwa kuwa mtakatifu kwa kipindi cha takribani miaka 50.

Mwana mfalme Wales alijumuika katika misa hiyo ambayo ilikuwa inawatambua wanawake wengine wanne kuwa watakatifu.


Mama Mariam Thresia kutoka India, Marguerite Bays kutoka Uswizi, Mama Giuseppina Vannini kutoka Italia na sista aliyezaliwa Brazili Dulce Lopes Pontes walikuwa wanatambuliwa pia kuwa watakatifu katika misa hiyo.

Mtakatifu John Henry Newman ni muingereza wa kwanza kutambulishwa tangu mwaka 1970
Maelfu ya waingereza walisafiri mpaka Rome ili kusheherekea utambulisho huo.

Carol Parkinson, katibu wa marafiki wa Newman kutoka mji wa Birmingham, anasema kuwa kutangazwa kwa mtakatifu huyo ni kwa kipekee na imekuwa siku ya hisia kubwa kwao.

“Uadilifu wake, urafiki wake, uaminifu pamoja na bidii aliyoweka katika kazi yake ni mfano mzuri wa kuigwa na kila mtu”, alisema.

Kadinali Newman alizaliwa mjini London mwaka 1801, alisoma chuo cha Trinity College na Oxford.

Alikuwa anatarajiwa kuwa padri wa kianglikana lakini alibadili dini na kuwa mkatoliki mwaka 1845.

Newman amesifika kwa miujiza miwili , muujiza wa kwanza ni kumponya mgonjwa wa uti wa mgongo wa kium na kumponya mwanamke aliyekuwa aachi kutokwa damu.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad