Papa Francis kukabiliwa na changamoto ya mapadri kuoa
0
October 07, 2019
Katika kipindi cha wiki tatu zijazo , wawakilishi 260 watazungumzia kuhusu mabadiliko ya tabia nchi , uhamiaji na Uinjilisti. ”Moto wa mungu una joto linalovutia na kuwakusanya kwa Umoja. Moto huo husambazwa kwa waumini na sio kupitia kujipatia faida”, alisema.
Lakini swala moja limetawala vichwa vya habari: Iwapo wanaume walio katika ndoa wataruhusiwa kuwa mapadri.
Mojawapo ya ajenda kuu katika mkutano huo ni pendekezo katika eneo la mashambani la Amazon , kwamba wazee, walio katika ndoa, wanaume, wanapaswa kufanywa kuwa mapadri.
Watahitajika kuwa wanaume wanaoheshimika na kulingana na stakhabadhi hizo watafanya kazi katika jamii wanazotoka.
Maaskofu wa Marekani Kusini wamepigania juhudi hizo ili kukabiliana na upungufu wa mapadri katika eneo hilo.
Mapadri tu ndio wanaoweza kumbariki Yukaristi, ambayo ni sehemu muhimu ya Misa.
Inakadiriwa kuwa karibu 85% ya vijiji huko Amazon haviwezi kusherehekea Misa kila wiki kwa sababu ya uhaba huu na wengine huonana na makuhani mara moja tu kwa mwaka.
Maaskofu wa kikatoliki duniani wanakutana katika mji wa Vatican kujadiliana hatma ya kanisa hilo katika eneo la Amazon.
“Papa Francis ambaye anatoka Marekani ya kusini ana uelewa wa changamoto za eneo hilo, kulingana na Profesa Gregory Ryan kutoka kituo cha cha mafunzo ya kikatoliki.
Wasiwasi wa ukosefu wa mapadri katika jimbo la Amazon ndio sababu ya tatizo hilo. Wakatoliki wanaamini kwamba Yukaristi ni swala la kila siku la jamii ya Wakristo.
Kwa wengi, kutoowa kwa mapadri ni mojawapo ya nguzo muhimu za kuwa padri.
Padri anafaa kufunga ndoa na Mungu na sio kusumbuliwa na kile ambacho wengine wanasema kuwa mke au familia.
Profesa Linda Woodhead, ambaye ni mtaalam wa maswala ya sosholojia ya dini anasema kwamba mbali na mapadri kutoowa, mapadri wa kikatoliki na watawa hupewa marupurupu ili waweze kujitolea katika kile wanachofanya.
”Watu uhisi kwamba mapadri wana muda wa kuwapatia na kwamba hawaingilii maisha yao ya faragha”, Profesa WoodHead anasema.
Padri yuko kuwahudumia wao na ni kitu maalum.
Kwa watamaduni, hili ni swala kuhusu mwelelekeo ambao papa Francis analipeleka kanisa lake.
Kadinali wa Ujerumani Walter Brandmueller ameripotiwa kusema kwamba mkutano huo wa Amazon unaweza ‘kuadhimisha kuporomoka kwa kanisa hilo’.
Wakosoaji wanalichukulia swala hilo la kuruhusu mapadri waliooa katika eneo la Amazon kama njia mojawapo ya kuondoa sheria hiyo ya kanisa hilo kwa jumla.
Wanashuku kuhusu pendekezo kwamba mkutano huo unaweza kutafuta kitengo ambacho kinaweza kupewa wanawake na hofu kwamba pia nao wanaweza kuanza kutawazwa kuwa mapadri.
”Lakini Profesa Wood Head anasema kwamba kanisa hilo hubadilika kama taasisi yoyote ile ambayo ina maisha marefu”, anasema.
”Limebadilika kiradikali tangu karne ya 20 . Lilikuwa likipinga demokrasia , uhuru na haki za kibinadamu . Na sasa linapigania haki za kibinadamu. Linabadilika mara kwa mara lakini kwa njia inayohitajika, anagongezea katika majadiliano na tamaduni zake”.
Ukweli ni kwamba tayari wapo?. Baadhi ya mapadri wa Kianglikana ambao walibadili dini na kuwa wakatoliki wakipinga kutawazwa kwa wanwake wameruhusiwa kuendelea na huduma zao.
Kanisa moja la mashariki pia lina mapadri waliooa. Kuna wengine ambao wanasema haiwezekani kwamba wanaume waliooa watatawazwa kuwa mapadri.
Linawezekana kufanyika katika maeneo mengine ambayo yanakabiliwa na uhaba wa mapadri kama vile kisiwa cha Pacific. Lakini profesa Ryan anahoji kwamba iwapo hilo litafanyika ,litafanyika kama jambo la kipekee.
”Kitu kimoja ambacho watu wana wasiwasi nacho ni kwamba je jambo hilo la kipekee litakuwa sheria?”, anasema. Nadhani kanisa halitakubali hatua hiyo kamwe. Utamaduni wa makuhani kutooa una mizizi katika kanisa katoliki.
Tags